Sturridge alisema kuwa kikosi chake kililalamikia kunyimwa penalti kadhaa katika kipindi cha kwanza na kueleza kwamba Koke alikuwa ameotea kabla ya kuipatia klabu hiyo ya Hispania bao la tatu.
Straika huyo aliipatia timu yake bao la mapema ambalo alilifunga kiufundi na kuifanya timu yake iende mapumziko ikiwa mbele kwa goli 1-0.
Timu hiyo iliyoko chini ya kocha Jurgen Klopp ilishinda kufanya vizuri katika kipindi cha pili na kuwapa nafasi Sevilla watawale mchezo katika fainali hiyo iliyofanyika kwenye mji wa Basle.
Kikosi cha timu hiyo tayari kimesharejea England kikitokea Ubelgiji kwenye fainali hizo.










