Mata: Tutabeba Kombe la FA

21May 2016
Na Mwandishi Wetu
LONDON, England
Nipashe
Mata: Tutabeba Kombe la FA

KIUNGO wa Manchester United Juan Mata amesema hana wasiwasi na timu yake kutwaa vikombe ndani ya miezi 12 ijayo kwa sababu ya morari ya ushindi waliyonayo.

Mashetani Wekundu hao hawajashinda kikombe chochote tangu 'Sir' Alex Ferguson alipojiuzulu 2013.

Hata hivyo, United ambayo imemaliza Ligi Kuu England ikiwa katika nafasi ya tano, leo inaweza kumaliza msimu kwa kutwaa ubingwa wa Kombe la FA endapo wataifunga Crystal Palace katika mechi ya fainali itakayochezwa leo.

"Klabu hii inaelekea kupambana kusaka vikombe," Mata aliiambia BBC michezo.

"Manchester United sasa akili yake ni kupata ushindi katika hali tofauti. Ninahakika klabu klabu itapambana kwa ajili ya kushinda kwa mara nyingine."

Mata amekiri wamesikitishwa na hatua ya timu yao kushindwa kupata nafasi ya kushiriki mashindano ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao lakini anaamini wataichukulia katika hali chanya kuelekea mchezo wa leo.

Mchezaji huyo raia wa Hispania alisema kuwa mchezaji aliye kwenye kiwango cha juu Marcus Rashford, ambaye amefunga mabao nane kati ya mechi 17 alizocheza na Anthony Martial watawasaidia kuwa na msimu mzuri baadaye.
BBC