Kinywaji hicho ambacho kimechanganywa na Vodka na kilicho tayari kwa ajili ya kutumika, kilizinduliwa kwa mara nyingine jijini Dar es Salaam baada ya kutokuwepo sokoni kwa kipindi huku kikitoa fursa kwa wasanii mbalimbali kutoa burudani.
Akiongea wakati wa uzinduzi huo, Meneja Uvumbuzi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Bertha Vedastus alisema pamoja na kuwaburudisha wateja wake na ladha nzuri na ya kipekee, kinywaji hicho pia kinajulikana kwa kuendeleza vipaji.
“Smirnoff Ice Black ni kinywaji kwa ajili ya kila mtu na pamoja na kuwaburudisha watumiaji wake, pia kimekuwa kikichangia katika kuibua na kukuza vipaji. Katika kipindi cha nyuma tumweza kufanya mashindano ya kutafuta Ma-DJ wakali na tulifanikiwa kufanya hivi mata tatu,” alisema.
Wakati kikirudi tena sokoni, Bertha alisema kinywaji hicho kitakwenda mbali zaidi kwa kuangalia vipaji vingine tofuati na Ma-DJ ili kuweza kutoa mchango mkubwa katika eneo hili ambalo limekuwa likisifika nalo.
Meneja uvumbuzi huyo aliwataka vijana wenye vipaji kuendelea kufuatilia kwa ukaribu taarifa mbali mbali kutoka Smirnoff ili kuhakikisha kuwa wanatumia fursa za kukuza vipaji zitakazo tangazwa.










