Mwanamuziki huyo ambaye amelamba dili nono la kuwa balozi wa nazi ya Azania ‘Azania Coconut Cream’amesema hayo juzi wakati wa uzinduzi wa bidhaa hiyo mpya kutoka katika kampuni ya Azania Group.
“Billnass anapenda sana wali maharage nazi, lakini sitaki sana kutoa siri za ndani asije mtu akapika wali maharage nazi bure ha ha ha ” alisema Nandy.
Nandy alisifia kiungo hicho cha nazi kuwa ni bora kuliko zingine alizowahi kuzitumia katika mapishi kwa kuwa kina virutubisho vya kutosha.










