Simba SC yafungiwa kusajili kisa Sakho

23Nov 2023
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Simba SC yafungiwa kusajili kisa Sakho

KLABU ya Ligi Kuu ya NBC ya Simba imefungiwa kusajili mpaka itakapolipa madai ya klabu ya Teungueth ya Senegal kuhusu Mchezaji Pape Ousmane Sakho.

Pape Ousmane Sakho.

Uamuzi ho umefanywa na Shirikisho la Kimataifa la Mira wa Miguu (FIFA) baada ya klabu hiyo kushinda kesi ya madai dhidi ya Simba kutokana na mauzo ya Sakho.

Kabla ya kujiunga na Simba, Sakho ambaye hivi sasa anachezea Timu ya Quevilly Rouen Metropole ya Ufaransa alikuwa Mchezaji wa Simba, Klabu hiyo ilifungua kesi FIFA dhidi ya Simba ikidai sehemu ya malipo kutokana na mauzo ya Sakho, Simba ilitakiwa iwe imetekeleza amuzi huo ndani ya siku 45 tangu ulipotolewa, lakini haikufanya hivyo.

Wakati FIFA imeifungia klabu hiyo kufanya uhamisho wa Wachezaji kimataifa, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeifungia Simba kufanya uhamisho wa ndani “TFF inazikumbusha Klabu kuheshimu sheria, kanuni na taratibu za mpira wa miguu ili kuepuka adhabu mbalimbali, ikiwemo kufungiwa kusajili Wachezaji”