Rais wa Simba, Evans Aveva alisema jana kuwa Milovan anataka kulipwa mshahara wa Dola za Marekani 12,000 (Sawa na Sh. milioni 24) ambazo klabu hiyo hazina.
Aveva alisema kuwa hiyo ndiyo sababu kubwa ya uongozi wake kushindwa kumrejesha kocha huyo aliyeingoa Simba katika ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Yanga kwenye mechi ya ligi 2011/12.










