Akizungumza katika hafla maalum ya iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam, Diamond alisema WCB ina wasanii 43 ambao shughuli zao za muziki zinasimamiwa na lebo hiyo akiwamo yeye mwenyewe.
Diamond alisema anatambua umuhimu wa msanii kuwa na lebo na yeye aliichagua WCB iliyoanzishwa mwaka 2010 chini ya Meneja, Hamis Taletale na Said Fella kuwa chini ya mikono yake.
"Si wanasiasa pekee wanaoweza kubadilisha maisha ya Watanzania, bali nyanja tofauti kwa nyakati zake wakiwamo wanamuziki wanaweza kufanya mabadiliko katika taifa, WCB inajaribu kuangalia ni namna gani shughuli za kimuziki zitaweza kusaidia vijana wenye vipaji mtaani," alisema Diamond.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basate), Goeffrey Mwingereza alisema kitendo alichofanya msanii huyo ni cha kuungwa mkono na wadau wa muziki.










