Kaimu Katibu wa Shimiwi, Moshi Makuka alisema ni vizuri timu hizo kutumia fursa hiyo kama sehemu ya maandalizi kwa ajili ya kushiriki michuano yake itakayofanyika Septemba mwaka katika mkoa utakayotangazwa baadaye.
"Tunaomba viongozi wa timu za Wizara na Idara mbalimbali kuanza maandalizi kwa kushiriki kwenye michezo ya Mei Mosi, hii itasaidia kujiimarisha na kuonyesha ushindani kwenye mashindano yetu ya Shimiwi," alisema Makuka.
Aliongeza kuwa uzinduzi wa bonanza la michezo ya Shimiwi litafanyika Mei mwaka huu kwenye uwanja wa shirikisho hilo uliopo eneo la Bunju, Dar es Salaam na mkutano mkuu Shimiwi utafanyika Desemba.










