Ligi ya kikapu hekaheka Dar leo

18Mar 2016
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Ligi ya kikapu hekaheka Dar leo

LIGI ya Kikapu Dar es Salaam inaanza leo kwenye Uwanja wa JK, Kidongo Chekundu jijini.

waziri, Nape Nnauye.

Rais wa chama cha mchezo huo Dar es Salaam (DARBA), Mwenze Kabinda alisema ligi hiyo itaanza kuchezwa kwa mtindo wa mtoano kutokana na timu nyingi kushiriki.

Kabinda alisema mfumo huo pia utasaidia kutoa nafasi kwa wachezaji kucheza mechi zaidi ya tatu kabla ya kufika hatua ya robo fainali.

Wakati huohuo, Kabinda alisema DARBA inatoa wito kwa utawala wa Jiji la Dar es Salaam kushirikiana na chama hicho kuandaa timu itakayofanya vizuri katika mashindano ya Majiji ya Afrika Mashariki yatakayofanyika Mei 16 na kuitumia fursa hiyo kulitangaza jiji na kuwapatia wafanyabiashara nafasi ya kuongeza uchumi wao.