Akizungumzia mchezo huo, Karatu mkoani Arusha, Kocha Mkuu wa Singida Fountain Gate, Hans van Pluijm, alisema wachezaji wake wameonesha kile anachokihitaji na kudai wameanza kuwa na muunganiko mzuri.
"Ninawapongeza wachezaji wangu wamefuata maelekezo niliyowapa tumefanikiwa kutoka na ushindi, hii ni ishara nzuri kuelekea mchezo wetu wa Ngao ya Jamii utakaotukutanisha na timu ya Simba," alisema Pluijm.
Alisema mchezo ulikuwa mgumu na wenye upinzani mkubwa kwani kila timu ilicheza vizuri kutokana na usajili zilizofanya.
Kwa upande wa Msemaji wa timu hiyo, Hussein Masanza, alisema maandalizi kuelekea Siku ya Singida (Singida Big Day), inayotarajiwa kufanyika Agosti 2, mwaka huu, yanaendelea vema na kwamba wataitumia siku hiyo kutangaza wachezaji wao ambao wamewasajili msimu huu.
"Tutatumia siku hiyo kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki, timu tutakayocheza nayo tutaitangaza muda wowote kuanzia leo," alisema Masanza.










