Mashujaa FC ambayo imepanda daraja msimu huu itafungua pazia la Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2023/24 kwa kuikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Parimatch Tanzania, Erick Gerald, wakati wa zoezi la utiaji saini wa mkataba ambalo lilifanyika kwenye ukumbi wa ofisi za klabu ya Mashujaa zilizopo jijini Dar es Salaam jana na kuhusisha viongozi wa pande hizo mbili.
Akizungumza jijini jana, Gerald alisema lengo la kuingia mkataba na klabu hiyo ni kukuza soko la mpira nchini pamoja na kuimarisha ushirikiano baina ya pande zote mbili.
"Parimatch tumekuwa wadau wakubwa katika sekta ya michezo hapa nchini na nje ya nchi, na kupitia udhamini huu unalenga kusaidia timu ambayo ina vijana wanaopata ajira, wanajenga afya na kuleta ushindani kwenye michezo," alisema Gerald.
Naye mwakilishi wa Mashujaa FC, Benjamin Kisinda, aliishukuru Parimatch Tanzania kwa kuwaamini na kuwaunga mkono.
Kisinda alisema udhamini ambao walioupata utawasaidia kupunguza changamoto za uendeshaji wa klabu yao.
Alisema timu yao inaendelea vyema na maandalizi na wamejipanga kuonyesha ushindani katika kila mechi ya Ligi Kuu Bara watakayocheza.
“Tunawashukuru wadhamini wetu Parimatch kwa kuja kuungana nasi katika kuendeleza soka, Mashujaa ni timu ambayo imepanda daraja msimu huu, kwa hivyo tunawakaribisha sana Kigoma katika familia ya Mashujaa,” aalisema Kisinda.
Kampuni ya Parimatch imekuwa ikijihusisha na kubashiri michezo mtandaoni na imekuwa ikitoa ofa kubwa ya bonasi ya ukaribisho ya 125% hadi kufikia Sh.milioni moja kwa wateja wapya wanaojiunga nao.
Parimatch imekuwa ikifanya kazi nchini Tanzania tangu mwaka 2019, ikitoa huduma nzuri ikijumuisha malipo ya haraka, odds kubwa na promosheni za kusisimua kwenye soka, Kasino na Michezo ya virtual. Mbali na soka, kampuni ya Parimatch pia hutoa mamia ya matukio kila siku kwenye tenisi, UFC, mpira wa vikapu, Kriketi, baseball na michezo mingine mingi ya Live na pre-match.









