...kwa kujipatia zawadi mbalimbali zikiwemo simu janja ‘Smartphone’ pamoja na fedha taslimu kiasi cha Shilingi milioni moja kila siku.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Masoko wa Parimatch Tanzania,Levis Paul wakati alipokuwa akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo leo na kusema kuwa Promosheni hiyo ni mahususi kwa wateja wao wote wa Parimatch wenye akaunti na hata wateja wapya watakaojiunga katika kipindi hichi cha Ligi zinaporudi.
Aidha, Levis amesema kuwa lengo kampeni hiyo ni kuwawezesha wateja wao kuendelea kucheza na kufurahia burudani kabambe kutoka kwako katika kipindi ambacho soka linarejea viwanjani ulimwenguni kote.
“Katika kipindi cha kuanzia 09.08.2023 hadi 08.09.2023, mteja wa Parimatch akifanya bashiri yake kwenye mchezo wowote kupitia tovuti yetu www.parimatch.co.tz au app zetu basi ataingia moja kwa moja katika droo wa kuwania pesa taslimu kiasi cha Milioni Moja za Kitanzania pamoja na smartphone aina ya Samsung mpya (Simu janja)”, alisema Levis.
Aidha Levis aliendelea kwa kusema kuwa “Kila siku tutakuwa tunatoa zawadi ya simu kwa washindi husika na Zawadi ya pesa itatolewa kila baada ya siku ya moja kupita. Washindi wote wanatangazwa kupitia Clouds fm katika kipindi cha michezo pamoja na kurasa zetu za kijamii kwa siku husika”.









