Baadhi wanabishana kuunga mkono hatua hiyo na wengine - akiwamo Kocha Xavi Hernandez – wakiamini mchezaji huyo wa Kimataifa wa Brazil hatafaa katika timu hiyo ya Barca.
Vyanzo vya klabu vinakataa kabisa uwezekano wa kurejea kwa mchezaji huyo wa PSG, ambaye aliondoka Barca mwaka 2017, lakini wanaonya kwamba litakuwa jambo gumu sana kifedha, na kwa sababu ya maoni tofauti juu ya kufaa kwake.
ESPN hapo awali iliripoti kwamba Neymar mwenye umri wa miaka 31, angefurahi kujiunga tena na Barcelona, na vyanzo viliongeza kwamba kwa mara nyingine ameongeza uwezekano huo katika siku za hivi karibuni.
Uwezekano wa kuhama ni mdogo, hata hivyo, kwa sababu ya matatizo ya kifedha ya klabu na upinzani wa Xavi kurejea kwake.
Zikiwa zimesalia siku nne tu Barca waanze msimu wao wa ligi wa 2023-24, wameshindwa kusajili wachezaji wao wapya - Ilkay Gündogan, Oriol Romeu na Inigo Martinez - au wachezaji ambao wameongeza mikataba yao hivi karibuni.
Kama matokeo, wana wachezaji 13 pekee wanaopatikana kwa mchezo wa Jumapili dhidi ya Getafe. Idadi hiyo inaweza kupunguzwa hadi 11 katika siku zijazo, huku Barca wakitarajia kukamilisha kuondoka kwa Franck Kessie kwenda Saudi Arabia na Ousmane Dembele kwenda PSG.
Klabu hiyo inafanya kazi kwa haraka kutatua tatizo hilo, na ujio wa Neymar utafanya hali kuwa ngumu zaidi, licha ya nia ya mchezaji huyo kuafikiana ili kufanikisha uhamisho huo.










