Ili kuhakikisha sekta hiyo inasonga mbele, amesema serikali itatunga sera mpya katika mwaka wa fedha 2016/17.'
Nnauye aliyetaja 'majipu' hayo kuwa ni uporaji wa kazi za wasanii, ujenzi duni wa miundombinu ya kazi za wasanii, usimamizi mbovu wa bodi ya filamu na tatizo la mfumo mbovu wa usambazaji wa kazi za wasanii.
Akizindua Tamasha la Filamu la Tanzanite International Film Festival (TIFF), Arusha juzi alisema jambo la kwanza atakalokwenda kulishughulikia ni wizi wa kazi za wasanii.
“Jipu la kwanza tutalitumbua kwenye bajeti yetu ya mwaka 2016/17. Jipu hili ni wizi wa kazi za wasanii,” alisema Nnauye
Alisema chini ya uongozi wake, atahakikisha anasimamia miundombinu bora ya ushambazaji wa kazi za wasanii ili wafaidike na jasho lao.Alisema mfumo wa kazi za usambazaji wa kazi za wasanii nchini pamoja na haki miliki ni wa kinyonyaji.
Rais wa Shirikisho la Wasanii wa Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifamba aliwataka wasanii wa filamui kujiandaa kisaikolojia kukabiliana na soko la ushindani wa filamu duniani kujenga utamaduni wa kuwa wabunifu.
“Tunaiomba Serikali iandae sera itakayoendana na mazingira mazuri kwa wasanii kuhusiana na usalama wa kazi zao,” alisema Mwakifamba.










