Mwanariadha Fabian Nelson aenda Japan

27Apr 2016
Renatha Msungu
Dar es Salaam
Nipashe
Mwanariadha Fabian Nelson aenda Japan

MWANARIADHA wa Fabian Nelson amewasili salama Japan kwa ajili ya kushiriki mbio za kusaka tiketi ya kucheza michezo ya Olimpiki zitakazofanyika Mei 7 nchini humo imeelezwa.

Mwanariadha Fabian Nelson akifanya maohijiano na mwandishi wa habari,;picha ya maktaba.

Nelson alienda mapema Japan ili aweze kufanya mazoezi na wanariadha wengine ambao watashiriki mbio hizo zinazotambuliwa na Shirikisho la Riadha dunaini (IAAF).

Akizungumza na gazeti hili jana, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya riadha, Francis John alisema mwanariadha huyo atashiriki mbio za mita 5,000 na akifanikiwa kufuzu ataungana na wenzake watatu ambao tayari wameshafuzu.

Alisema mwanariadha huyo anaendelea vizuri na mazoezi na tunatarajia atafanya vyema kwenye mbio hizo na kupeperusha bendera ya Tanzania katika michezo ya Olimpiki itakayofanyika Agosti nchini Brazil.