Hayo yamesemwa na viongozi wa Chama cha Mpanda Veterani sports Clabu ambacho kwasasa kina wanachama zaidi ya 50 ambao wameungana kwaajili ya kuhakikisha michezo inasongambele ndani ya mkoa huo.
"Matarajio yetu sisi kama Mpanda Veterans nikuhakikisha tunaimarisha umoja wetu, kuwa chanzo cha kuhamasisha wadau wengine kujihusisha na michezo hasa mpira wa miguu tunataka tulee vipaji ili tupate wachezaji watakao cheza mbali zaidi,"amesema Katibu wa Chama hicho Hussein Athumani.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Katavi Kenneth Pesambili amesema wakotayari kushirikiana na Clabu hiyo ili kupata kikosi bora kitakacho wakilisha mkoa wa Katavi kwenye mashindano ya mpira wa miguu.









