ITALIA. Jose Mourinho atakuwa anawafuatilia nyota wawwili wa Inter atakapotembelea San Siro wakati akijiandaa kutua Manchester United.
Kocha huyo wa zamani wa Chelsea, ataishuhudia timu yake ya zamani wakati wa mechi yao dhidi ya Sampdoria katika mechi ya Serie A na anatarajiwa kuwafuatlia straika Mauro Icardi na beki wa pembeni Miranda.
Taarifa zinadai kuwa Mreno huyo yuko tayari kukisuka upya kikosi cha United atakapotua Old Trafford kumrithi Louis van Gaal. (La Stampa)










