Pambano hilo la raundi 12 litafanyika Jumamosi kwenye Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini jana, Meneja wa Cheka, Juma Ndambile, alisema maandalizi yote yamekamilika na Waziri Nape amekubali ombi la kuwa mgeni katika pambano hilo.
Ndambile alisema mpinzani wa Cheka atawasili nchini Jumatano huku wawakilishi wa Shirikisho la Ngumi la Dunia (WBF) ambao wataongozwa na rais wao, Goldberg Haward, watatua Alhamisi.
Aliongeza kuwa kabla ya pambano kuu, kutakuwa na mapambano ya utangulizi huku pia bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta' ikitarajiwa kutoa burudani.
"Napenda pia kuwaambia mashabiki wa ngumu kuwa Cheka yuko 'fiti' na hajawahi kuwaangusha Watanzania akiwa hapa nyumbani," alisema.
Hii itakuwa ni mara ya pili kwa mabondia hapo kupigana baada ya mwaka 2008 kuzidunda nchini England na Cheka kupigwa kwa pointi.









