Baada ya kufanikiwa kumdhibiti vyema mshambuliaji hatari wa Simba, Hamis Kiiza, Pato alisema jana kuwa hakukamia mechi kama inavyodaiwa na baadhi ya mashabiki na kwamba kilichotokea Jumamosi ndiyo uchezaji wake na ataendelea nao.
"Hata usifikiri kuwa kocha alinipa kazi ya kwenda kumkaba Kiiza, ila mimi ni mchezaji na najua wajibu wangu na nilikuwa natekeleza wajibu," alisema mchezaji huyo.
"Lakini ilikuwa mechi ngumu. Ilikuwa mara yangu ya kwanza (kucheza mechi ya watani wa jadi) na nashukuru kuanza kwa kucheza vema na tumeshinda," alisema.
Beki huyo pia alikiri kuwa kumkaba kinara wa mabao katika Ligi Kuu Tanzania Bara kwa sasa, Kiiza kunahitaji nguvu na utulivu wa hali ya juu pamoja na kutompa nafasi ya kujiandaa.
Pato alipata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga Jumamosi kutokana na kuumia kwa nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro' huku beki wa kati Kelvin Yondani akimalizia adhabu ya kukosa mechi tatu baada ya kulimwa kadi nyekundu katika kipigo cha 2-0 dhidi ya Coastal Union Januari 30.
Katika mechi ya Jumamosi, Yanga ilishinda 2-0 na kuweka rekodi ya kuwa timu ya pekee iliyoshinda mechi zote mbili dhidi ya Simba msimu huu.










