Hadi sasa, Kamati ya Nidhamu ya Simba, hajafanya uamuzi wowote, lakini kuna taarifa kuwa 'hukumu' yake itatolewa baada ya mchezo wa ligi kuu leo kati ya Simba na Toto Africans.
Banda anadaiwa kuonyesha utovu wa nidhamu mbele ya kocha wake, Jackson Mayanja.
Uongozi wa Simba ulimtaka mchezaji huyo kujieleza kwa kosa hilo, lakini pamoja na kufanya hivyo hadi sasa hakuna uamuzi uliotolewa.
Mbali na suala la Banda, wachezaji wengine, Hamis Kiiza na Juuko Murishid nao wameingia kwenye kikaango cha madai ya utovu wa nidhamu.
Wachezaji hao wanatarajia kuwekwa kitimoto kwa kuchelewa kuripoti kambini baada ya kupewa ruhusu na uongozi.
Msemaji wa Simba, Haji Manara
alisema jana kuwa kamati nidhamu itakutana baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi Toto Africans.
"Kwa sasa tunawekeza nguvu kwenye mechi inayofuata, masuala ya utovu wa nidhamu wa wachezaji tunauweka kando kwa muda," alisema Manara
Simba imendolewa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho, hivyo nafasi pekee iliyobaki kucheza michuano ya Klabua Afrika ni kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Simba inaongoza ligi kwa tofauti ya pointi moja dhidi ya Yanga inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi 56, ikifutiwa na Azam FC yenye pointi 55. Timu hizo mbili zilitarajiwa kushuka dimbani jana kucheza mechi zao za ligi kuu.










