Nape: Migogoro Stand United inakera

17Apr 2016
Marco Maduhu
Shinyanga
Nipashe Jumapili
Nape: Migogoro Stand United inakera

WAZIRI wa Habari, Michezo, Utamadani Sanaa na Wasanii, Nape Nnauye ameonya kuwa mgogoro wa uongozi unaofukutaka kwenye timu ya Stand United utaipoteza timu hiyo.

waziri wa Habari, Michezo, Utamadani Sanaa na Wasanii, Nape Nnauye.

Nape alisema hayo katika ziara yake ya mikoa ya kanda ya ziwa na kubainisha kuwa, tatizo kubwa ni 'ulaji' unaosababishwa na viongozi wabovu.

Alisema ili mambo yarejee kwenye hali ya kawaida, lazima ufanyike uchaguzi wa kuchagua viongoz wapya.

"Timu haina viongozi wa maana ndiyo maana imeandamwa na migogoro kila kukicha. Nimeambiwa pia kuwa viongozi waliopo siyo halali," alisema Nape.

Katika hatua nyingine Nape alisema wizara yake itasimamia na kuimarisha uongozi kwenye vyama vya michezo ili vyama hivyo vijiendeshe ka faida.

"Naamini kama vyama vya michezo vikijiendesha kwa kufuata katiba na kusimamia uongozi bora na kujitenga na migogoro, maendeleo ya michezo yanaweza kupatikana," alisema.