Tajiri huyo maarufu, ni mgombea wa urais katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Novemba mwaka huu.
Katumbi ambaye amewahi kuwa gavana wa jimbo la Katanga alijiuzulu na kumshtumu rais wa sasa wa DRC, Joseph Kabila, kwa uongozi dhaifu.
Sawia na viongozi wengine wa upinzani, Katumbi amemsihi rais Kabila, kutokiuka katiba ya nchi hiyo kwa kuacha madaraka wakati muhula wake wa pili utakapomalizika Desemba mwaka huu.
“Jambo la muhimu kwa wakati huu, sio kuwa rais, jambo muhimu kwetu ni katiba iheshimiwe, na mamlaka ya nchi ikabidhiwe kwa mshindi kwa njia ya amani nchini DRC, na pia kalenda ya uchaguzi kuheshimiwa, na pia kuunganisha upinzani.
''Nafahamu raia wa nchi hii wana matarajio makubwa kutoka kwangu, na sasa tutaketi ili kumchagua mmoja ambaye atakuwa mgombea wa pekee wa upinzani,” alisema Katumbi ambaye anatajwa kusimama kwenye kiti hiko.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa Shirika la Habari Uingereza (BBC), Katumbi ni kiongozi wa pekee wa upinzani nchini Kongo ambaye ana ushawishi mkubwa na ufuasi mkubwa miongoni mwa raia wa Kongo na anayetarajiwa kuumpa rais Kabila ushindani mkali endapo atawania tena.










