Ngasa atoswa Stars, Kazimoto, Msuva warejeshwa

09Mar 2016
Na Mwandishi Wetu
Dar
Lete Raha
Ngasa atoswa Stars, Kazimoto, Msuva warejeshwa

KOCHA wa ‘Taifa Stars’ Charles Boniface Mkwasa amewarejesha kikosini kipa Shaaban Kado na kiungo Mwinyi Kazimoto, huku akiwatema nyota wa Yanga, beki Nadir Haroub 'Cannavaro' na winga Simon Msuva katika kikosi chake ambacho kitaikabili Chad Machi 23.

Mrisho Ngassa.

Katika kikosi cha wachezaji 25, Mkwasa pia amemtema mchezaji mzoefu kiungo mshambuliaji wa Free State Stars ya Afrika Kusini, Mrisho Ngasa, wakati hakujaribu kumuita aliyekuwa nahodha wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wa Yanga, ambaye alitangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa baada ya kuvuliwa unahodha bila ya taarifa.

Akitangaza kikosi hicho katika mkutano wa waandishi wa habari kwenye ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mkwasa aliwaomba wachezaji aliowaita katika kikosi hicho kujiweka fiti kwenye mazoezi wanayoyafanya katika klabu zao, kwani hakutakuawa na muda wa kufanya mazoezi kwa ajili ya mechi hiyo ya ugenini.

“Nasisitiza wachezaji niliowachagua wahakikishe wanajilinda wenyewe kwa kuwa fiti wanapokuja kwenye safari ya mchezo huo wa machi 23, 2016,” alisema Mkwasa.
Wachezaji 25 walioitwa kwa ajili ya mchezo huo ni:

Makipa
Aishi Manula (Azam FC), Ally Mustapha 'Barthez' (Yanga SC) na Shaaban Kado (Mwadui FC)

Mabeki
Juma Abdul, Haji Mwinyi, Kelvin Yondani (Yanga SC), Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, David Mwantika (Azam FC) na Mohamed Hussein (Simba SC)

Viungo
Himdi Mao (Azam FC), Ismail Juma (JKU), Jonas Mkude, Said Ndemla, Mwinyi Kazimoto (Simba SC), Mohammed Ibrahim, Shizza Kichuya (Mtibwa Sugar), Farid Mussa (Azam FC), Deus Kaseke (Yanga SC).

Washambuliaji
Mbwana Samatta (nahodha, KRC Genk Ubelgiji), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC), John Bocco (Azam FC), Elias Maguri (Stand United), Jeremia Mgunda (Tanzania Prisons) na Ibrahim Hajib (Simba SC).