Mashindano hayo yalifanyika katika mikoa ya Mwanza, Mbeya, Arusha na Dar es Salaam.
Lengo la mashindano hayo ni kukuza vipaji ambapo timu hizo nne zitashindana na kutoa timu moja itakayojulikana kama Safari Champions – mabingwa wapya katika mpira (The New Order of Champions).
"Timu hizo nne zilizopatikana zitaingia kambini mapema mwezi ujao na baadaye kushindanishwa ambapo wachezaji 22 watachaguliwa ili kuunda timu ya Safari Lager Champions itakayocheza na moja ya timu kubwa katika ligi kuu ya Tanzania",.
Makocha Jamhuri Kihwelo na Sekojo Chambua wanasema hili ni zoezi la aina yake na lenye lengo la kuongeza tija katika tasnia ya mpira.










