Mwakinyo kupitia wakili wake, Azadi Athumani ametoa ombi hilo, leo Novemba 20, mwaka huu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Amiri Msumi, baada ya kuitikia wito wa Mahakama.
Katika kesi hiyo ya madai namba 227/2023, kampuni ya PAF Promotion imewasilisha madai nane, likiwemo la kumtaka bondia huyo kuilipa Sh milion 150 kama hasara waliopata baada ya bondia huyo kushindwa kupanda ulingoni tofauti na mkataba wake aliosaini.
Kampuni hiyo imemfungulia Mwakinyo kesi hiyo baada ya kushindwa kupanda ulingoni katika pambano lililoandaliwa na kampuni hiyo, lililokuwa limepangwa kufanyika Septemba 29, 2023 jiji hapa kwa kile alichonukuliwa akisema ni waratibu hao kukiuka masharti ya makubaliano.









