Hans Pope ainanga TFF

16Apr 2016
Faustine Feliciane
Dar
Nipashe
Hans Pope ainanga TFF

HUKU hatima ya kashfa ya upangaji matokeo katika mechi mbili za Ligi Daraja la Kwanza ikiwa halijamalizika, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu ya Simba, Zacharia Hanspope amesema Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), litapoteza wadhamini wa Ligi Kuu kama hatua za haraka za hazitachukuliwa.

Zacharia Hanspope.

Kauli hiyo ya Hanspope imekuja baada ya wadhamini wa Ligi Kuu, Kampuni ya Vodacom kusema wanasubiri kusikia hatua zitakazochukuliwa dhidi ya wahusika ili kulinda heshima yake.

Akizungumza na kituo kimoja cha redio, Hanspope alisema hakuna kampuni itakayokubali kutoa fedha zake katika mchezo wenye matokeo 'haramu'.

"Kama hakuna hatua za haraka zaidi za kukemea mambo haya, tunaweza kuwakosa wadhamini," alisema kiongozi huyo.

Aliongeza kuwa ili kujenga taasisi na maendeleo ya mchezo, viongozi wa TFF walipaswa kuwajibika ili kulinusuru soka la Tanzania.