Matola ambaye aliwahi kuichezea na kuifundisha Simba alisema, “Ningependa timu yangu ipangiwe kucheza dhidi ya Simba kwasababu ninaipenda Simba lakini pia ninataka kuifunga.
“Simba imenilea kama mchezaji na kama kocha lakini ilishindwa kuniamini hivyo ningependa kutumia Kombe la Shirikisho kuwaonesha mimi ni kocha wa aina gani.
“Nataka kuonesha nina uwezo gani na kwanini Simba huwa hawaniamini licha ya kuwa ninaipenda timu hiyo.
Nafahamu kuwa droo za robo fainali zitapangwa na kama sitapata nafasi ya kukutana na Simba, nitapambana na ile timu nitakayobahatika kupangwa nayo na hivyo kazi itakuwa ni kusaka ushindi tu,” alisema kocha huyo.
Geita ambaye inatarajia kupanda Ligi Kuu msimu ujao baada ya kumaliza Ligi ikiongoza kundi C la Ligi hiyo huku wakihusishwa na upangaji matokeo walifanikiwa kuitoa Toto African kwenye michuano hiyo baada ya kuifunga bao 1-0 na kutinga robo fainali.
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura alisema kuwa droo ya robo fainali itapangwa mwishoni mwa wiki hii na zoezi hilo litakapomalizika mechi za robo fainali zitachezwa siku za mwisho za wiki ya tatu ya mwezi huu.










