Bingwa wa mashindano hayo, ataiwakilisha Bara kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.
Habari za ndani zinadai kuwa, droo hiyo itaonyeshwa live na kituo cha televisheni kinachodhamini mashindano hayo.
"Droo itachezeshwa Alhamisi, itakuwa 'live' katika kipindi cha Alasiri," kilisema chanzo chetu.
Timu nane zimefuzu hatua hiyo, ambazo ni Simba, Yanga, Azam FC, Coastal Union, Ndanda FC, Mwadui FC , Prisons zinazoshiriki Ligi Kuu ya Bara na Geita Goldmine FC ya Ligi Daraja la Kwanza.










