Cheka alishinda kwa pointi katika pambano ambalo mpinzani wake alikataa kukubali matokeo yake.
Akizungumza jana, Cheka alisema ataupeleka mkanda huo kwa Magufuli kama alama ya kuitaka Serikali kusaidia kukuza mchezo huo.
"Naupeleka mkanda wa ubingwa huu kwa Rais Magufuli. Mimi na mwenzangu (Cheka Cosmas) tumefuata nyayo za Mbwana Samatta kuiletea sifa Tanzania," alisema Cheka.
Alisema ushindi wake angependa kuona unakuwa kiini cha kuwaamsha mabondia wengine kujituma kwa ajili ya taifa.
Kwa upande wa Cosmas Cheka, alisema ubingwa wa WBF Afrika alioupata ni mwanzo mzuri kwake.
Mkurugenzi wa Advanced Security, Juma Ndambile alisema ameamua kuwekeza nguvu nyingi kusaidia mchezo wa ngumi nchini.










