Bondia Majiha kupanda ulingoni Juni 30

08May 2023
Saada Akida
DAR ES SALAAM
Nipashe
Bondia Majiha kupanda ulingoni Juni 30

BONDIA wa ngumi za kulipwa Tanzania, Fadhili Majiha 'Stopper' anatarajia kupanda ulingoni Juni 30, mwaka huu katika pambano ambalo Mfaume Mfaume atacheza na Nkululeko Mhlongo raia wa Afrika Kusini kwenye pambano kuu.

 

Pambano hilo ambalo limeandaliwa na PAF Promotion Entertainment Company LTD linatarajia kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Akizungumza na Nipashe jana,  Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Fadhili Maogola alisema  tayari washamalizana na Majiha kwa ajili ya kucheza pambano hilo na kwa sasa wanajipanga kumalizana na mpinzani wake ambaye bado hajawekwa wazi.

 “Hakuna ambaye hajui ubora na ukubwa wa Majiha akiwa ni bondia anayekamata nafasi ya pili katika mabondia bora Watanzania kwa sasa, kilichobakia kwa sasa, tunaweka mipango na mikakati yetu vizuri na kuweza kumalizana na mpinzani wake,” alisema Mkurugenzi huyo.

Alisema hawawezi kuweka wazi jina la mpinzani wa Majiha kwa sababu ya mambo ya kibiashara hadi watakapokuwa wamemalizana kwa kusaini mkataba kwa ajili ya pambano hilo.