MKONGWE wa muziki wa kizazi kipya, Ambwene Yesaya ‘AY’ amesema kuwa wakongwe wenzake wanatakiwa kukubaliana na mabadiliko kwenye muziki huo ili waweze kufanya vizuri zaidi.
Amesema kuwa muziki unaenda na wakati, hivyo wasanii wanatakiwa kukubaliana na usasa huo ili waweze kupiga hatua zaidi kwenda mbele badala ya kubaki wakiwalaumu tu.
"Tunatakiwa kukubaliana na mabadiliko kwenye muziki wa kizazi kipya ili tuweze kufanya vizuri kwenye gemu badala ya kulalamika tu ama kulaumu bila kuangalia hali halisi ya sasa," amesema AY.
'AY' ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya wa Zogo remix aliomshirikisha Diamond Platnumz, ni miongoni mwa wasanii wakongwe ambao hawajashuka kwenye soko la muziki huo.
Sababu kubwa ya msanii huyo kuendelea kuwa matawi ya juu inatokana na jinsi ambavyo anafanya kazi zake kulingana na mazingira na mabadiliko ya muziki huo yanavyokwenda.










