Nacho Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kimetaka serikali kuchukua hatua stahili kwa vitendo dhidi ya tishio la kuibuka kwa wimbi la tatu la corona.
Katika maeneo ya huduma za afya wananchi wanatakiwa kuvaa barakoa kwa lazima, huku baadhi wakipunguza idadi ya watu wanaotembelea wagonjwa na wanaokwenda kwa ajili ya kliniki kwenda wenyewe.
Hadi sasa hakuna takwimu zilizotolewa rasmi na serikali kuonyesha hali ya maambukizi na vifo, huku kukiwa na shinikizo la mashirika ya misaada ya kimataifa kutaka nchi kuweka wazi takwimu zake.
Hatua ya serikali kusema wazi kuna tishio la wimbi la tatu ni nzuri na sasa nguvu kubwa ielekezwe kwenye elimu kwa wananchi, kwa kuwa mtaani watu wanaendelea na maisha kama kawaida bila tahadhari yoyote dhidi ya corona.
Kwenye vyombo vya usafiri wa umma watu wanapanda kwa kujazana na hakuna uvaaji wa barakoa, huku kwenye masoko na maeneo ya mikusanyiko hakuna tahadhari zozote muhimu ikiwamo kunawa mikono.
Rais Samia Suluhu Hassan, aliunda kamati ya wataalamu ili kuishauri serikali, na ilishatoa taarifa yake na kupendekeza nchi kukubali chanjo, lakini iwe ni hiari.
Tayari Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, limesema limepokea ombi la Tanzania kuingizwa kwenye mpango wa chanjo za corona, ingawa Msemaji wa serikali alikaririwa akisema kuwa taarifa itatolewa baada ya Baraza la Mawaziri kujadili mapendekezo ya kamati.
Kwa upande wa Zanzibar, Rais Hussein Ali Mwinyi, alisema watapokea chanjo na itakuwa hiari, na sasa tahadhari imetolewa na Waziri wa Afya kwa kuwataka watu kujikinga.
Kwa ujumla ni muhimu serikali ikaweka wazi takwimu ili kuonyesha uhalisia wa ukubwa wa ugonjwa huu nchini na kuwalazimisha wananchi kuchukua tahadhari.
Rais Samia ameonyesha kwa mfano kwa kuvaa barakoa kila mkutano au aendako huku wanaohudhuria kikao au mkutano wako kuwa wamevaa, ni jambo linalopaswa kuigwa na sekta nyingine.
Mathalani, bungeni kuna mkusanyiko mkubwa na ingepaswa waonyeshe kwa mfano uvaaji wa barakoa, ili kuhamasisha wananchi kuvaa, na hilo kitafanikiwa zaidi kwa kuwa wawakilishi wa wananchi watatuma ujumbe moja kwa moja kuwa kuvaa barakoa ukiwa kwenye mikusanyiko ni muhimu.
Aidha, kasi ya kutoa elimu kwenye maeneo ya mikusanyiko kama minada, masoko, mikutano na vikao mbalimbali ingeongezeka ili kudhibiti kasi ya kusambaa kwa ugonjwa huo.
Wataalamu wanaeleza kuwa virusi hivyo hubadilika muundo kadiri siku zinavyosonga, na ndiyo maana India ilikumbwa na aina mpya ya kirusi hicho, huku Uganda ikiingia katika awamu ya pili.
Bila kusisitiza umuhimu wa kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni kama ilivyofanyika mwaka jana, baada ya serikali kutangaza uwapo wa virusi hivyo, wananchi wataendelea kuzembea na hali itakuwa mbaya zaidi.
Nguvu sasa iongezwe kutoa elimu ya corona
23Jun 2021
Mhariri
Dar es Salaam
Nipashe
Nguvu sasa iongezwe kutoa elimu ya corona
SERIKALI za Jamhuri ya Muungano na Zanzibar zimetoa tahadhari dhidi ya mlipuko mpya wa janga la corona, na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari kuhakikisha wanakuwa salama muda wote.










