Babu Colin Dunn (84) na Bibi Sally Smith (82), walifikia makubaliano hayo, baada ya kuzungushana kimapenzi tangu mwaka 1972.
Colin alikuwa anafanya kazi jirani na baa moja ambako Sally alikuwa anafanya kazi. Walikutana mara nyingi siku za wikiendi, Colin akifika baa kuburudika.
Ni harusi ya aina yake, ambayo sherehe yake ilihudhuriwa na marafiki wasiopungua 100 na ilifanyikma katika klabu moja jijini hapa, ambako walipata mlo na harusi ilifungwa katika Kanisa la Mtakatifu Mary.
Sally anasema alichumbiwa mwaka jana akiwa na umri wa miaka 81 na mumewe zamani alikuwa dereva wa lori na sasa ni mstaafu.
“Sally alikuwa ananihudumia kila wikiendi nikifika baada ya kazi,” anasimulia Colin kukumbusha mwanzo wa mapenzi yao na anaongeza:”Tulikuwa ‘tunachati’ na hatimaye tulitoka out.”
Wapenzi hao waliamua kuona wakiwa na watoto wanne, mdogo kuliko wote ni mwenye umri wa miaka minne.
Colin anasema: “Suala la ndoa halikuniingia kabisa kichwani. Mara nyingi tulikuwa tumetingwa na malezi ya watoto au kwenda kwenye sikukuu.
“Ghafka tukajikuta watoto wanakuwa na wanaondoka nyumbani, nikijikuta mimi na Sally pekee ndio tumebaki. Tukaona umefika wakati wa kuwa mume na mke.”
“Lakini tulijikuta tukisema ‘itakuwa mwakani, itakuwa mwakani’ tukiwa na furaha,” anaongeza Colin.
Ni maamuzi yaliyofikiwa wanandoa hao ‘wabichi’ wenye wajukuu 13 na vitukuu tisa.
Colin anasema: “Kabla ya Kirismas nilimpoteza kaka yangu na muda mfupi kabla ya hapo, nilimpoteza kaka mkubwa zaidi.
“Tulikuwa tunapitia kipindi kigumu na tukaanza kuulizana, hivi hili likitokea kwa mmoja wetu itakuwaje? Tukaamua kwamba tunahitaji kuwa mume na mke.”
Ndoa hiyo ilifungwa katika Kanisa la Mtakatifu Mary iliyoko jijini hapa na baada ya hapo, wakaenda kupata mlo.
“Ni subira yenye thamani. Siku yenye upendo hata kwa hali ya hewa. Tulikuwa na keki nzuri katika sherehe,” anasema Sally huku akidakiwa na Colin anayesema:
“Ilikuwa (sherehe) ya kupendeza. Kulikuwapo watu wengi waIiotusaidia kusherehekea. Kila kitu kilienda sawia mithili ya mshale wa saa.”
Anasema penzi lake sasa limenoga zaidi ya siku aliyomuona Sally kwa mara ya kwanza. Anafafanua: “Kama unafanyia kazi uhusiano, utaendelea kudumu. Amekuwa akinijali nami namjali.”
Babu huyo anaongeza: “Ni jambo dogo kwangu akisinzia, ninamuamsha akalale kitandani. Ninamuandalia chakula na chai.”










