Wanasoka wa5 wanaofanana kiuchezaji na Ronaldo

27Mar 2023
Na Mwandishi Wetu
UINGEREZA
Nipashe
Wanasoka wa5 wanaofanana kiuchezaji na Ronaldo

CRISTIANO Ronaldo ni mmoja wa wanasoka bora wa wakati wote. Alianza kung’ara mapema miaka ya 2000 kama winga mwenye ujuzi mwingi wa mchezo huo. Kwa sababu ya kujitolea kwake kabisa, nidhamu na bidii, alifurahia kupanda kwa haraka kwenye kilele cha ubora.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37, ana mtindo wa kucheza sahihi na inaonekana wazi jinsi anavyocheza, chenga au kupiga mipira ya adhabu.

Mshindi huyo mara tano wa Ballon d'Or bila shaka amekuwa kivutio cha wanasoka wengi. Kumwiga mwanasoka unayempenda ni jambo la kawaida sana.

Wanasoka chipukizi wanajaribu kuiga mchezo kwa wanasoka wanaowapenda.

Hapa tunwaangalia wanasoka watano ambao wana mtindo wa uchezaji sawa na Cristiano Ronaldo, twende sasa...

 

#5 Son Heung-Min (Tottenham Hotspur)

Son Heung-Min ni mojawapo wa vipaji vya hali ya juu kwa kizazi chake. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Korea Kusini amekuwa mmoja wa washambuliaji thabiti katika Ligi Kuu England kwa miaka kadhaa sasa. Son alishinda Kiatu cha Dhahabu cha Ligi Kuu msimu uliopita kwa pamoja na Mohamed Salah wa Liverpool.

Mtindo wa uchezaji wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30, unafanana kabisa na ule wa Ronaldo. Yeye yuko moja kwa moja na mpira miguuni mwake na anapenda kuwafuata mabeki na kuwapiga chenga. Kama Ronaldo katika siku zake za ujana, Son anacheza kama winga wa kushoto ambaye anaweza kupiga mpira kwa miguu yote miwili.

Alijiunga na Spurs mwaka 2015, akitokea Bayer Leverkusen kwa kitita cha euro milioni 30. Kwenye mechi 348 katika mashindano yote kwa miamba hao wa London Kaskazini, Son amefunga mabao 137 na kutoa asisti 76.

 

#4 Memphis Depay (Barcelona)

Kama Ronaldo, Memphis Depay, aliwasili Manchester United akiwa winga mchanga ambaye alikuwa na uwezo wa kuwa mshindi wa dunia. Hakuwa na nafasi nzuri kabisa Old Trafford, lakini alionyesha kung'ara kwa uwezo wake wakati alipokuwa huko.

Ilikuwa kule Olympique Lyon ambapo Depay alifanikiwa kujiimarisha kama fowadi wa ubora wa juu. Ustadi wa Mholanzi huyo wa kucheza chenga ni wa kustaajabisha na unamkumbusha sana Ronaldo wakati wa miaka yake kuu. Yeye pia ni bora katika upigaji mashuti kutoka winga na pia ni mpigaji mzuri wa mipira iliyokufa 'free-kick'.

Kutokana na hali hiyo, uchezaji wa Depay mara nyingi umekuwa ukifananishwa na ule wa Ronaldo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, kwa sasa hapewi nafasi sana kule Barcelona kwani Wakatalunya hao wana utajiri katika idara ya ushambuliaji.

 

#3 Joao Felix (Chelsea)

Joao Felix ana mtindo wa kucheza unaofanana kabisa na Ronaldo. Ingawa Ureno imetoa washambuliaji wengi wenye vipaji katika miaka ya hivi karibuni, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, anatajwa kama ana siku bora zaidi zinazokuja.

Furaha ilikuwa kubwa kiasi kwamba Atletico Madrid ilimsajili Felix kutoka Benfica mwaka 2019 kwa kitita cha euro milioni 126. Kwa kawaida hutumika kama mshambuliaji wa pili katika mfumo wa Diego Simeone. Ubora wa Felix upo kwa wote kuona, lakini makubaliano yanaonekana kuwa labda Simeone si kocha sahihi kwake.

Sasa amejiunga na Chelsea kwa mkataba wa mkopo hadi mwishoni mwa msimu huu. Felix ni gwiji wa mbele mwenye sifa bora za kiufundi. Uchezaji wake wa kuchezea, ubunifu na upigaji mashuti unaonekana kama ule wa Ronaldo.

 

#2 Marcus Rashford (Manchester United)

Marcus Rashford kwa sasa anacheza katika ubora wake. Kwa kiwango cha sasa, yeye ni mmoja wa washambuliaji bora duniani. Ustadi wake wa kuchezea chenga ni wa hali ya juu na kasi yake ya kusisimua inamruhusu kumpita karibu kila beki anayekutana naye.

Rashford amekuwa Manchester United tangu akiwa na umri wa miaka saba na ni wazi ametengeneza mchezo wake baada ya gwiji wa klabu hiyo, Ronaldo. Mwingereza huyo ni mmoja wa wapiga chenga waliobobea zaidi kwenye sayari hii na hata mara kwa mara anatumia staili ya Ronaldo kuwavaa wapinzani.

Mara nyingi anatumia mbinu ya kupiga chenga na kupiga mipira ya adhabu na ni mtindo ambao ulipendwa na Ronaldo.

 

#1 Kylian Mbappe (Paris Saint-Germain)

Kylian Mbappe ndiye mshambuliaji bora zaidi duniani kwa sasa. Alishinda Kiatu cha Dhahabu kwenye Kombe la Dunia la FIFA la 2022 na hata alifunga hat-trick katika fainali ya mashindano hayo. Mbappe alifichua katika mahojiano na Marca mwaka 2017 kwamba Ronaldo alikuwa kipenzi chake utotoni na kwamba alionekana kuiga mtindo wake wa kucheza akiwa mtoto.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24, anapendekezwa kufikia au hata kuvuka urithi wa shujaa wake huyo wa utotoni. Kasi yake ya kusisimua na uwezo wa kupiga mashuti humfanya kuwa fowadi hatari sana. Ni ndoto ya kujilinda dhidi yake na ni mmoja wa wachezaji wanaotafutwa sana kwenye mchezo hivi sasa.