Wanafunzi sekondari wabuni chombo kinachofyonza vumbi kielektroniki

11May 2023
Renatha Msungu
DODOMA
Nipashe
Wanafunzi sekondari wabuni chombo kinachofyonza vumbi kielektroniki
  • • Wasifu; gharama nafuu, kusiko umeme inatumika

SERIKALI inasisitiza kuibuliwa vipaji mbalimbali kwa vijana chipukizi wa kike na kiume, ili kuviendeleza vilete matokeo chanya kitaifa, ikiwamo kuwaandaa wajiajiri, huku mwelekeo kisera nao ukichukua njia hiyo.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari St Peter Claver, iliyopo Ihumwa, Dodoma wakiwa katika maonyesho ya Wiki ya Ubunifu, iliyomalizika hivi karibuni, katika Uwanja wa Jamhuri, mjii Dodoma. PICHA ZOTE: RENATHA MSUNGU.

 

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolijia, kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) katika kutekeleza hilo imekuwa ikiandaa mashindano yaitwao MAKISATU yanayoenda sambamba na Wiki ya Ubunifu kitaifa.

Lengo ni kuibua vipaji vya wabunifu wachanga, pia zitambulike kitaifa na kimataifa kuja kuonyesha bidhaa zao, zinazoshindanishwa katika kundi husika, kumsakla mshindi, pia ikiwa ni namna ya kuvutia wabunifu wachanga kujitokeza kuwasilisha mawazo yao yafanyiwe kazi, sasa kukionekana mafanikio.

Katika mashindano hayo, nafasi ya kwanza mwaka huu imeenda kwa Chuo cha Ufundi Arusha au Arusha Tech, ya pili Shule ya St, Peter Claver, ambayo ubunifu wake ulijikita kwenye kifaa cha kusafisha mazingira, kufyonza vumbi kwa njia ya kielektroniki.

 

UBINIFU ULIVYO

Mmoja wa timu ya wabunifu, Patricia Mhilu anayesoma kidato cha nne, anasema waliamua kubuni mfumo huo kurahisisha jamii kuweka mazingira safi, katika maeneo wanayoishi na ofisini.

Kwa mujibu wa Patricia akizungumza, sababu kubwa iliyowafanya wabuni mashine hiyo ya kuondoa vumbi, ni kutaka jamii kuweka mazingira safi kwenye nyumba wanazoishi na maeneo mengine, kutokana na kuwapo changamoto ya vumbi inayoleta athari nyingi za kiafya.

Anasema wakaanza kwa utafiti mdogo kudadisi tatizo lililoko, wakarejea shuleni na kubuni njia mbadala inayosaidia kuondoa vumbi, badala ya kutumia vitambaa kufuta kama ilivyozoeleka kwa jamii nyingi.  Hapo ndio ukawa mwanzo wa kufyonzwa na kusafishwa vumbi.

“Sehemu kubwa ya jamii inatumia vifaa kama vitambaa kwa ajili ya kukung’uta vumbi, suala ambalo linatumia muda mrefu. Lakini, ukitumia mashine hiyo, inakusaidia kutumia muda mchache kusafisha sehemu kubwa ya mavumbi yaliyopo ndani,” anasema Patricia.

Hapo anafafanua kwamba, wamebuni wazo na wamelifanyia kazi kwa kuonyesha mashine, sasa wanaiomba serikali kufuatilia ubunifu waliol nao uendelezwe na Kutambulika, kwa manufaa ya sasa na baadae.

Mwanafunzi Victoria Nchilla, anasema mashine walioibuni ya kufyonza vumbi, hadi sasa ina faida kubwa kwa kwa jamii, akiisifu ina gharama nafuu, nzuri na inaweza kutumika sehemu yoyote ile, kutokana na kutumia betri na umeme ili kuweza kufanya kazi.

Anasema ni mashine inayoweza kutumika kwa wakazi wa vijijini na mjini, kwa sababu inatumia betri, hata kuwafaa jamii iliyoko vijijini, ambayo bado haijaunganisha umeme kwenye makasio yao.

“Hii bunifu ni nzuri sana na inahitaji kuendelezwa ili iweze kupiga hatua na kutambulika kimataifa, kwa sababu ina faida kubwa na inaweza kutumika mijini na vijijini,” anasema Nchilla.

 

MAMLAKA YA SHULE

Buberwa Karongo ni Mkuu wa Shule  anasema shule inatambua umuhimu wa vipaji vya wanafunzi na ndio maana wamewaruhusu kwenda kushiriki katika maonyesho mbalimbali ya ubunifu, ili wajifunze zaidi

kutoka kwa wanafunzi wa shule nyinginezo. Karongo anafafanua, pia wanahitaji kuona mwanafunzi anakuwa mzuri katika masomo ya vitendo nje ya darasani na ni moja ya sababu zao, kuwapa elimu ya ubunifu vijana hao, wakiwaandaa kujiajiri katika mustakabali wa baadae.

Pia, mkuu huyo wa shule, anaishIkuru serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolijia, kwa kuandaa Wiki ya Ubunifu, akiamini inasaidia kuwajenga

vijana katika somo la ubunifu, ambalo hulifanya kwa vitendo, kutokana na mawazo yao wanayayowasilisha kwa walimu yakaidhinishwa, kabla ya kuwasilishwa katika Maonyesho ya Wiki ya Ubunifu.

Anasema ni hali inayosaidia kuwajengea uwezo wanafunzi, ikiwamo kuwapa muda wa kubadilishana mawazo na wanafunzi wa shule nyinginezo, kitendo kinachowasaidia kupanua wigo wa ubunifu ambao unapoendelezwa, unarejesha matokeo chanya kwa wote.

Mkuu wa Taaluma wa shule hiyo, Jeannette D’mello, anaishauri serikali kutenga bajeti kwa wanafunzi wa shule za sekondari wenye uwezo  kubuni mifumo ya kuondoa changamoto kwa jamii, ili kuwasaidia kukuza vipaji vyao na kuingia kwenye soko la ushindani.

D’mello anasema, vipaji vya wanafunzi wanavyovionyesha katika makongamano na wiki za ubunifu katika maeneo mbalimbali wakiwa bado chipukizi, kama walivyofanya vijana wake, inapaswa kuendelezwa kadri siku wanavyozidi kukua.

Anasema shule yake ina dira ya kumtengeneza mwanafunzi katika nyanja tofauti, ikiwamo iliyobnazishwa ya usafi wa mazingira, kwa ajili ya faida yake siku zijazo. Anendelea: “Tumekuwa tukiwafundisha darasani wanafunzi wetu kwenye kitengo cha Sayansi na vitengo vingine, wanafunzi wamekuwa wakibuni vitu mbalimbali na walimu kuwasimamia, ili ubunifu wao uboreshwe na kuingia katika mashindano au maonyesho ya ubunifu,”

 

WAZIRI PROF. MKENDA

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, anawataka wabunifu kutobweteka na ushindi walioupata, badala yake wapige hatua zaidi, kwa kile walichokibuni mwaka huu, ili mwakani kiweze kuendelezwa na kufikia ngazi ya kimataifa. 

Profesa Mkenda anayasifu maonyesho ya sasa, yamekuwa bora zaidi, kwa sababu wengi walioshirikishwa,  ubunifu wao ama umetimia au

ulishaendelezwa na serikali na kutambulika kimataifa, hivyo wasisite kubuni bidhaa bora wawavutie wabunifu wachanga  kujitokeza katika maonyesho tajwa.

 

 

Top of Form

Bottom of Form

Top of Form

Bottom of Form