SIKU YA MAZINGIRA AFRIKA:Hatujafanikiwa kutunza mazingira – Dk. Ningu

03Mar 2016
Christina Mwakangale
Dar
Nipashe
SIKU YA MAZINGIRA AFRIKA:Hatujafanikiwa kutunza mazingira – Dk. Ningu

LEO ni siku ya mazingira barani Afrika, Tanzania ikiwa sehemu mojwapo.

Wakazi wa kijiji cha Gombero,Kata ya Kibirashi wakiangaika na kero ya Maji.(Picha ya mtandao)

Lengo la kuadhimisha siku hiyo ni kukumbusha na kuhamasisha jamii, kuhusu umuhimu wa kutunza na kuhifadhi mazimgira.

Changamoto kubwa kwa karne ya 21 inayokabili nchi zinazoendelea, ikiwamo Tanzania, ni uharibifu wa mazingira ambao kwa asilimia kubwa unatokana na binadamu.

Uchafuzi wa mazingira unaoendana na utupaji taka ovyo mitaani, katika vyanzo vya maji, ufugaji wa kuhamahama, kuwa idadi kubwa ya mifugo, kwa njia ya kilimo na ukataji miti holela, kumesababisha upotevu wa bioanuai na kuleta mabadiliko ya tabianchi.

Ongezeko kubwa la watu hususan katika maeneo ya mjini, ni changamoto nyingine, kwani sensa ya watu na makazi nchini ya mwaka 2012, inatajan idadi ya Watanzania inakaribia watu ni milioni 45.

Idadi hiyo inawelezwa kukaribia mara mbili zaidi ya idadi ya watu kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita. Makadirio yaliyopo ni kwamba ,ifikapo mwaka 2035, idadi ya Watanzania watakuwa milioni 100.

Usimamizi wa sheria ya mazingira na kanunu zake ni sababu nyingine kutokana na na ongezeko la shughuli za kiuchumi, ujenzi holela wa makazi mjini inaleta pingamizi la sheria hii.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, asilimia 60 ya eneo la Tanzania lipo katika hatari ya kugeuka jangwa.

Mkurugenzi wa Mazingira katika Ofisi ya Makamu ya Rais, Dk. Julius Ningu, anataja baadhi ya mikoa iliyoko hatarini ni Singida, Dodoma, Simiyu, Shinyanga, Mwanza na Kilimanjaro.

Anasema ukame huo unatawaliwa na hali ya kukauka vyanzo vya maji, uhaba wa chakula, mambo yanayofanya uchumi wa wakazi kuporomoka.

Dk. Ningu anasema kuwa uwajibikaji mdogo wa mamlaka za miji na halmashauri katika ukusanyaji taka zinazozalishwa kila siku, hasa mjini, unaongeza uchafuzi wa mazingira.

Dk. Ningu anasema mlundikano wa taka hizo umesababisha kuwapo magonjwa ya mlipuko, ikiwamo ugonjwa wa kipindupindu.

Anarejea Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004, inaeleza jinsi ya kutunza mazingira hasa kwa wasimamizi, yaani halmashauri, sekta mbalimbali na taasisi.

Dk. Ningu anasema mabadiliko ya tabianchi yanayosababishwa na shughuli za kibinadamu, kama vile matumizi ya nishati ya mkaa na kuni, inahitaji kuwa na mikakati mbadala inayotunza mazingira na misitu.

Anatoa mfano wa nchi zinazoendelea kuwa zinapaswa kushinikiza nchi zilizoendelea, zipunguze uzalishaji wa hewa ukaa inayotoka katika viwanda vikubwa.

USAFI
Anasema mkakati mwingine wa serikali ni kufanya usafi kitaifa kila Jumamosi ya mwisho ya kila mwezi, ili kuweka mazingira katika hali ya usafi.

Jingine analosema, ni serikali imesitisha usajili wa viwanda vya kutengeneza mifuko ya plastiki na kwa sasa inayotakiwa ni yenye upana na anayoitaja kuwa ‘micro’ 50 badala ya 30.

“Mifuko hii ikiwa na kiwango cha chini, inapeperuka na kusafiri umbali mrefu na kusababisha uchafuzi wa mazingira. Pia mtumiaji anatumia mara moja tu, kwa kuwa ni mwepesi na huchanika haraka,” anasema Dk. Ningu.

MIKAKATI YA MKOA
Dodoma ni kati ya mikoa inayokumbwa na njaa kila mwaka kutokana na ukame. Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa, anasema hivi mpango mkakati nuliopo ni kuahakikisha kilimo cha uzalishaji mazao yanayostahimili ukame kinafanyika.

Anasema pia utumiaji mahindi kwa ajili ya kutengenezea pombe, unapigwa marufuku ili kutunza mahindi kwa ajili ya chakula.

MATUKIO YA VIFO
Kutokana na uchafuzi wa mazingira, inakadiriwa watu milioni 5.5 wanapoteza maisha duniani kila mwaka, kutokana na maradhi mbalimbali, ikiwamo yatokanayo na mfumo wa hali ya hewa, saratani, kipindupindu na homa za matumbo.