Namna uzito wa mwili inavyopunguzwa

03Mar 2016
Na Mwandishi Wetu
Dar
Nipashe
Namna uzito wa mwili inavyopunguzwa

Ili mtu apunguze uzito wa mwili wake anapaswa kufanya maozezi ya mara kwa mara. Imekuwa jambo la kawaida watu wakichukua hatua za kudhibiti uzito wao kwa kufanya mazoezi katika maeneo maalum, kukimbia na aina ya mazoezi yanayofanana nayo.

Mazoezi ya kupunguza uzito.

Pg 21

Tayari imejengeka utamaduni kutoka kwa baadhi ya watu kwamba kila inapofika mwaka mpya, miongoni mwa mikakati ya watu wengi ni namna gani wanavyopunguza uzito ndani ya msimu mpya wa mwaka.

Mtaalam wa afya na mtafiti kuhusu mazoezi ya mwili, Profesa Coneel Vandelanotte anaorodhesha njia kadhaa za kupunguza uzito na kujenga afya ya mwili.

Mtafiti huyo wa afya kutoka Chuo Kikuu cha Queensland nchini Australia, analenga mahsusi katika upunguzaji uzito, akiorodhesha mbinu kadhaa zinazopaswa kutumika.

Anasema njia ya kwanza ya kupunguza ni kufanya mazoezi ya mwili na viungo na kuhakikisha kunakuwepo uwiano sahihi kuhusu nishati ya mwili kwa kile kinacholiwa na namna kinavyotumika.

Profesa Coneel anasema kuwa uzito wa mwili unapungua kwa kuendana na namna mwili unavyoshughulika.
Chuo kimoja cha Afya cha nchini Marekani kupitia utafiti wake, kinasema kuwa ili mwili wa mtu ufanikishe kupunguza uzito wake, unapaswa kushughulika kwa kipindi cha kati ya dakika 250 (saa nne na dakika 10) na dakika 300 (saa tano).

Inaelezwa kuwa, ili mtu awe na afya bora, anapaswa kufanya mazoezi ya mwili kwa walau kwa dakika 30 kwa siku.
Wataalam wanasema kuwa namna mtu anavyomudu kupunguza uzito kwa kiwango kinachostahili, mazoezi ni kitu muhimu, tendo linalounganishwa na kusimamia chakula kwa namna sahihi kwa mwongozo wa ushauri wa kitaalam.

Faida ya pili ya kufanya mazoezi ya mwili ni kwamba, anaieleza kuwa mtu anaondokana na maradhi ya shinikizo la moyo, kansa na mengineyo.

Maozezi yanaelezwa na wataalam kuwa yanamuweka mtu mbali na vitambi, uzito mkubwa na kifo cha mapema.
Mtazamo wa tatu unaoelezwa na mtaalam huyo ni kwamba unafaa kufuatwa katika kupata afya njema na mhusika hapaswi kufanya mazoezi ya mwili kwa kutumia nguvu sana hata akaumia, jambo linalomfanya ashindwe kufanya baadhi ya mambo kama kupumua na kuzungumza.

Profesa coneel anasema kuwa, badala yake anatakiwa kufanya mazoezi taratibu kama vile kuendesha baiskeli, hali ambayo hutoa majibu bora yanayotarajiwa kama vile kwenye afya ya mwili.

Jambo la tatu linalohimizwa katika mazoezi ya mwili, katika kufanya mazoezi hayo yanatakiwa kuwa ni ya aina inayogusa sehemu kubwa ya viungo vya mwili na mtu aweze kupumua na kutokwa jasho.

Pia aina hiyo ya mazoezi inaelezwa kutokuwa na uhusiano wowote na kusababisha maumivu ya mwili.

Jingine la nne linaloelezwa ni kupitia mazoezi ya mwili, misuli ya mwili inahitaji nishati zaidi kuliko uwepo wa mafuta.
Na ili misuli ifanye kazi hiyo, inatakiwa izoeshwe kuendeleza mazoezi hayo ya mara kwa mara hata kupunguza uzito kwenye misuli na kuifanya iwajibike inavyopaswa.