Lijue penzi la kweli na masharti yake tisa

15Mar 2016
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Lijue penzi la kweli na masharti yake tisa

Dhana ya mapenzi ni tata na ina tafsiri pana sana katika maisha. Kuna wasanii wa muziki wanaonena kwamba: “mapenzi ni neno dogo, lakini ina tafsiri pana.”

Katika hali ya kawaida, inaangukia katika namna nyingi, ikiwemo kwenye uhusiano wa ama kijinsia au kindugu.

Ili kufanikisha mapenzi ya kweli, wanasaikolojia wamebaini mitazamo tisa inayopaswa kuzingatiwa kwa umakini.

Moja, ni kumpata mbia sahihi katika kupendana na kuwa wawazi na wakweli katika kutatua kinachoendelea kati ya wawili. Nia isiyo sahihi inapotosha na kujenga kasoro kubwa.

Pili, ni kujenga mipaka juu ya yale unayoyasimamia katika mapenzi hata kabla ya kuingia katika uhusiano huo na mara zote kuzingatia yale ya kuyaamini.

Tatu, mapenzi yanapaswa kuingizwa wakati wote na mawasiliano na kauli nzuri zitawale katika mawasiliano hayo

Nne, penzi la kweli linatajwa kuwa na malengo na utashi wa kufikia malengo hayo kwa pamoja na utashi wa mtu mmoja mmoja.

Mpenzi anatakiwa ainishe yote yanayolenga kuyatimiza katika maisha na kile ambacho mwenza wako anakihitaji, kisha wasaidiane katika matumizi.

Tano, ili mtu ajue kuwa na penzi la kweli mara zote, anapaswa kujifunza kutenganisha penzi na mambo mengine yanayomhusu kwa karibu kama vile ya familia, marafiki na wafanykazi wenzake.

Ili kufanikisha penzi, mhusika anatakiwa kuwa na heshima, mkweli, muwazi na anayekujali kwa namna zote.

Sita, aliyeko katika mapenzi saa zote ajiondoe katika hali ya kujishuku anaonewa na hana mamlaka katika maamuzi ya yale yaliyoko kwenye uhusiano.

Saba, ndani ya uhusiano wa mapenzi kinachotakiwa ni kuishi kwa malengo na kutumia muda mwingi katika namna ya kuishi ndani ya penzi hilo.

Nane, kutambua na kutekeleza kuwa mapenzi katika mwongozo kwamba, penzi la kweli halina chembe inayomdhuru mtu katika sura ya kero na hali inayofanana na hiyo.

Tisa, penzi la kweli halimshurutishi mwenza katika mapenzi, aachane na yale anayopenda katika maisha, kama vile kutumia vinywaji vya aina fulani na kushiriki michezo.