Dunia yote inafatilia kwasababu rais wa Marekani uonekana kama rais wa dunia kutokana na nguvu za nchi hiyo kiuchumi na kijeshi na mara nyingi maamuzi yake huwa yanagusa maisha ya watu wengine ulimwenguni hata kama wao si wamarekani na hata kama hawakuhusika katika kumchagua .
Kama tunavyo fahamu mchakato wa uchaguzi wa rais wa Marekani uanzia kwenye vyama vya siasa ambapo wanachama wanaotaka kugombea nafasi ya urais hulazimika kutafuta ridhaa ya vyama vyao na kuomba kupewa nafasi ya kugombea nafasi hiyo nyeti kwa tiketi ya vyama vyao.
Mchakato wa kumpata mgombe wa kupeperusha bendera ya chama uanzia kwa kutafuta ridhaa ya wanachama katika majimbo yote ya nchi hiyo kupitia kura za maoni.
kupitia utaratibu wao mgombea utafuta kupata zaidi ya nusu ya idadi ya kura za wajumbe wawakirishi wa majimbo wote wanaotokana na mgawanyo wa uwakirishi uliopangwa kwa kila jimbo.
Si nia yangu kueleza kwa undani mambo ya mchakato huu katika makala haya lakini itoshe kusema kwamba mchakato wa kuwapata wagombea watakao teuliwa na vyama kugombea nafasi ya urais wa Marekani mwaka huu unaedelea kwa sasa na unafatililiwa kwa karibu na dunia nzima.
Kama tunavyofahamu Marekani kwa miaka mingi ni nchi inayotumia mfumo wa siasa wa vyama vingi lakini ikiwa na vyama vikuu viwili vinavyopishana katika kutwaa madaraka na kuendesha serikali. Vyama vikuu hivi ni chama cha Democrat na kingine ni chama cha
Republican.
Nimelazimika kusema mambo ya uchaguzi wa Marekani kwa sababu nataka tujadili mambo ya yanayotokana na kauli tata mbili za wanasiasa moja akiwa ni Bwana Donald Trump yule anayekusanya kura za maoni za chama cha Republican ili kimteue kugombea urais kwa tiketi yachama hicho katika uchaguzi wa mwaka huu wa rais wa Marekani.
Jambo la pili nataka tuangalie mtazamo wa mwanasiasa kutoka Zanzibar ambaye ni Balozi Ally Karume na siasa za urais wa Zanzibar. Baadaye tuangalie kauli hizo zinamaana gani katika uongozi barani Afrika kwa ujumla
Sasa ni takribani miaka 23 tangu kurudi mfumo wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini Tanzania.
Zanzibar kama Marekani imekuwa na vyama viwili vikuu vya siasa vinavyo uchuana kwa ushindani mkubwa katika uchaguzi mkuu kila unapofanyika ambavyo ni CCM na CUF kama inavyokuwa mchuano mkali kati ya vyama vya Democrat na Republican vya Marekani.
Hata hivyo tofauti na Marekani mpaka sasa Zanzibar chama kilicho fanikiwa kutangazwa mshindi na kuchukua dola ni kimoja yaani chama cha mapinduzi CCM.Mara zote matokeo ya uchaguzi huwa yamekaribiana mno kiasi cha kuleta mvutano kila upande ukidai kuwa wao ndiyo washidi halali.
Kwa bahati mbaya uchaguzi wa mwaka jana haukuwa tofauti, mvutano ulikuwa mkubwa kiasi cha kwamba Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar iliamua kufuta matokeo yote ya uchaguzi katika mazingira ya kutatanisha.
Sasa katika mazingira kama hayo, Karume aliandika makala katika gazeti akisema kwamba rais wa Zanzibar awe anachaguliwa kutoka CCM pekee daima!
Hoja anayoitoa katika kujaribu kuhalalisha kauli yake ni kwamba hiyo ndiyo njia ya kulinda mapinduzi ya Zanzibar.
Aidha, Karume amejaribu kuonyesha kwamba Cuf ni chama chenye uhusiano na watawala waliopinduliwa katika mapinduzi matukufu ya Zanzibar na hivyo wakiachiwa kutawala basi watamrejesha Sultani.
Kauli hii inashangaza na kusikitisha sana kwa sababu nyingi. Moja ni aiba ya mtu aliyeitoa na nafasi yake katika jamii. Huyu ni kiongozi na pia ni mtoto wa kiongozi wa kwanza wa Zanzibar huru.
Aidha, amekuwa balozi aliyewakilisha nchi yetu kwa miaka mingi katika mataifa mengine.
Kusikia kauli ya kibaguzi na ya kikandamizaji kama hii, kauli inayoikataa demokrasia na kuashiria udikteta wa hali ya juu kutoka kwa mtu wa aina yake siyo tu inasikitisha bali pia inaudhi.
Hakuna hata chembe ya shaka kwamba Karume angependa Zanziba itawaliwe kiimla.
Inatukumbusha stori ya Animal firm ambapo baada ya kumpindua binadamu kutoka katika utawala wa shamba la wanyama kwa kisingizio kwamba binadamu alikuwa anawatesa na kuwanyonya, wanyama walioendesha mapinduzi waligeuka na kuanza kufanya mambo yale yale ya kikandamizaji aliyokuwa akiyafanya binadamu na kwa ubaya zaidi.
Kauli hii inanikumbusha swali alilopata kuuliza hayati Mwalimu Nyerere wakati akihoji uhalali wa baadhi ya mataifa kupinga hatua ya kumchapa Idd Amini wa Uganda kwa kuvamia nchi yetu kwamba itakuwaje tumkumbatie mtu anayevamia waafrika wenzake, na kuwatesa wananchi wake kwa ukatili mkubwa eti tu kwasababu ni mtu mweusi lakini tuwachukie na kuwagombeza
Makaburu wa Afrika ya Kusini kwa kufanya vitendo kama hivyo ili hali wao ni watu weupe? Kwa lugha nyepesi Mwalimu alichukia udhalimu bila kujali rangi ya mdhalimu.
Kwa hiyo basi mimi pia nataka nikatae hapa ubaguzi wa Karume bila kujali kama yeye ni kiongozi au mtoto wa baba wa taifa la Zanzibar.
Haiwezekani baada ya miaka 52 ya mapinduzi kupita na watu wa Zanzibar kuwa huru kutokee mtu anayedhani anaweza kuwaondolea uhuru wao kwa kuwabagua na kutaka wajisikie kama wao si sehemu halali ya watu wa nchi yao.
Kauli ya Karume
Inashangaza kwa vile inawataka wananchi wa Zanibar wakubali kutawaliwa kiimla na CCM.
Hapa tunasema tutapinga kwa nguvu zetu zote kwa sababu hatuangalii kama anayetawala kiimla ni mweusi au mweupe. Utawala wa kiimla unakataliwa bila kuangalia rangi, kabila, dini au chama.
Sasa Karume na wengine wengi wenye mawazo kama yake wanataka kuturudisha kwenye utawala usiyo wa kidemikrasia kwa kisingiio chakulinda mapinduzi anayodai yalipatikana kwa gharama kubwa.
Labda tumkumbushe Karume kwamba mapinduzi anayoyatetea hayana maana hata kidogo kama hayakuleta uhuru wa kweli kwa wazanzibari.
Uhuru wa kweli ni pamoja na wananchi wote bila kubaguliwa kupata haki yao ya msingi ya kuchagua au kuchaguliwa kuwa viongozi. Mapindunzi yakishindwa kulinda haki za msingi za raia basi hakuna haja ya kuwayafanya maana itakuwa yale yale ya ekaya za animal firm.
Aidha tunajua siku zote madikteta mahali popote duniani hawaishi kutoa visingizio vya kupoka demokrasia.
Mfano mzuri ni rais wa Zimbabwe Bwana Robert Mugabe ambaye ameendelea kung’ang’ania madarakani kwa karibu miongo minne sasa kwa kisingizio kwamba analinda ardhi ya waafrika wa Zimbabwe isitwaliwe na wazungu wachache.
Na kaenda mbali zaidi kwa ‘kuhonga’ wapiganaji wake ardhi ili tu aendelee kulindwa na aendelee kutawala kwa kutumia mbinu chafu za kuiba matokeo ya uchaguzi na za kudhoofisha upinzani.
Kwa mawazo ya Karume inaonekana vitendo vya kuvuruga uchaguzi ili mradi ‘kulinda’ mapindzi ni mufaka kwake. Lakini ukweli ni kwamba vitendo hivi vinaturudisha nyuma na kutudharau mbele ya jumuiya ya kimataifa.
Imefikia mahala ambapo watu ndani ya bara la Afrika wameachana na shughuli za upigaji kura maana wanaona ni kama kupoteza muda maana matokeo yatachezewa ili huyo anayelinda maslahi ya wachache waliofanikisha kumuweka madarakani aendelee kutawala.
Kuna kipindi tulidhani kwamba Tanzania tuko salama na nchi yetu inaheshimu misingi ya demokrasia na utawala wa haki. Sasa hivi hayo si kweli tena.
Vituko vilivyofanyika Zanzibar katika uchaguzi uliopita vinadhihirisha haya. Mbaya zaidi mawazo ya watu kama Karume yameanza kushamiri na kufagiliwa na kutekelezwa na wakubwa walioshika dola.
Ni jambo hatari na la kufedhesha kwa sababu tunarudi katika ukoloni na ubeberu wa waafrika wenzetu.
Ni kwasababu hii nashawishika kukubaliana na kauli ya Bwana Trump. Inasemekana kwamba katika moja ya mikutano yake ya kampeni ya kuwania kuteuliwa na chama chake cha Republican ili apeperushe bendera ya chama hicho katika uchaguzi wa rais wa Marekani .
Trump alitoa kauli kwamba Afrika mambo yetu ni bado sana na ili kuiweka sawa inatakiwa itawaliwe na wakoloni kama mwanzo kabla ya kujitawala wenyewe au ikombolewe upya.
Licha ya kwamba Trump ni mbaguzi na ametoa kauli nyingi tata kiasi cha kuzusha mjadala mkali juu ya baadhi ya misimamo yake lakini kwa hili inaonekana hayuko mbali na ukweli kutokana na tunayoyashuhudia ndani ya bara hili na mawazo mgando kama ya akina Karume.
Viongozi wengi Afrika sasa wanataka kuendele kutawala maisha hawataki tena demokrasia ya kuachiana madaraka.
Wengine wanalazimisha matokeo yachezewe ili vyama vyao vishinde.
Hatawakishindwa katika uchaguzi wanatumia mbinu chafu wanabadilisha matokeo ili wabaki madarakani.
Viongozi wetu wanabadili katiba ili waruhusiwe kuendelea kubaki madarakani.
Angalia Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe kafanya hivyo. Njoo kwa majirani zetu Uganda na Rwanda rais Yoweri Museveni na Paul Kagame wamefanya hivyo. Burudi ndiyo kwanza mzozo wa mambo haya umeshika kasi. Rais Paul Bia wa Cameroon mambo ni yale yale.
Wengine walitamani kufanya hivyo na wakajaribu ila walishindwa. Hawa ni pamoja na rais wa zamani wa Zambia bwana Chiluba.
Hata hapa kwetu ilihitajika nguvu ya ziada kumzuia komandoo Salmin Amour.
Aidha, baadhi yaviongozi wengine wanaolazimika kuondoka wanataka wapandikize watu wao watakao walidia maslahi yao. Rais Kikwete alijaribu pia lakini bahati haikuwa yake maana sote tunakumbuka mnyukano wa kumpata mgombea kwa tiketi ya CCM u;ivyokuwa.
Ni kwa sababu ya mambo kama haya tunadhani kwamba Trump na wengine wote wanaopenda uhuru wa kweli wanaona viongozi Waafrika wameanza kujitengenezea mazingira kama yale ya stori ya Animal firm.
Kibaya zaidi hata hawaleti maendeleo kwa watu. Mtindo wa utawala wao ni wakujinufaisha kwa kupora mali na rasilimali za nchi na kujilimbikizia mabilioni na matrililoni ya dolla nje.
Katika mazingira kama haya mtu atashawishika kukubaliana na Trump kwamba au tukombolewe tena kwa sababu sasa tumetawaliwa na ukoloni wa waafrika wenzetu wanaotunyonya wazi wazi na kutubagua na kutunyima hata haki za msingi kama vile elimu, afya, uhuru wa kujieleza na uhuru wa kuchagua viongozi tunaowataka au kuchaguliwa.
Maana kama nilivyokwishaeleza udhalimu ni udhalimu hauwezi kuwa mzuri eti kwakuwa umefanywa na mwafrika mwenzetu.
Hata kama hatutohitaji kutawaliwa tena na wakoloni kutoka nje ya bara letu la Afrika lakini nadhani kwa mawazo ya akina Karume tutahitaji kujikomboa kwa mara nyingine kwa vile watawala wetu wameamua kurudisha ukoloni wa kiafrika na kama mabwana wakubwa Nguruwe wa Animal firm wanafanya mabaya zaidi ya wakoloni wa kizungu na wamekuja na staili ya










