katika kukabiliana na vitisho vinavyoongezeka kutoka kwa maadui wake, vyombo vya habari vya serikali vilisema jana.
Kauli hizo, zilizotolewa na shirika rasmi la habari la Korea Kusini (KCNA), zimeweka bayana hali ya wasiwasi inavyozidi kuongezeka kwenye rasi ya Korea baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuweka vikwazo vipya dhidi ya taifa hilo Jumatano iliyopita kutokana na programu yake ya nyuklia.
Korea Kaskazini, inayojulikana sana kwa kauli kali, hapo awali ilitishia kuanza kuzishambulia nchi maadui zake, zikiwamo Korea Kusini na Marekani.
Wataalamu wa masuala ya kijeshi wana mashaka kama nchi hiyo tayari imeshajijengea uwezo wa kufyatua kombora la masafa marefu lenye silaha ya nyuklia kuweza kufika Marekani.
Kim alitoa kauli hizo alipokuwa akisimamia mazoezi ya kijeshi yaliyohusisha mizinga mipya iliyoboreshwa ya kufyatulia maroketi, KCNA iliripoti.
Hata hivyo, shirika hilo halikugusia tarehe iliyofanyika mazoezi hayo lakini lilisema Korea Kusini ni kati ya sehemu ambazo zimo ndani ya umbali unaofikiwa na silaha hizo mpya.
Wizara ya ulinzi ya Korea Kusini ilisema juzi kwamba Korea Kaskazini ilifyatua makombora kadhaa kutokea kwenye pwani yake kuelekea baharini umbali wa hadi kilomita 150 (maili 90), ikionekana dhahiri kuwa ni jibu kwa vikwazo hivyo vya Umoja wa Mataifa.
Kim alisema Korea Kaskazini inapaswa "kuboresha nguvu yake ya nyuklia kwa ubora na wingi wake" na kusisitizia "haja ya silaha za nyuklia zilizowekwa kwa ulinzi wa taifa daima kuwa katika hali ya tahadhari ili ziweze kufyatuliwa muda wowote," KCNA ilimnukuu kiongozi huyo akisema.
Kiongozi huyo pia alisisitizia haja ya jeshi kujiandaa kuwa katika hali ya kuweza kukabiliana na maadui zake kwa kuanza kufanya shambulizi.









