HARUNA NIYONZIMA; Kasi mpya, nguvu kibao

15Feb 2016
Faustine Feliciane
Dar
Nipashe
HARUNA NIYONZIMA; Kasi mpya, nguvu kibao

TAKRIBANI mwezi mmoja na nusu uliopita, kiungo 'fundi' wa Yanga, Haruna Niyonzima tayari alionyeshewa mkono wa kwaheri na klabu yake ya Yangao kutokana na vitendo vyake vya utovu wa nidhamu.

Haruna Niyonzima.

Hata hivyo, baada ya mvutano wa muda mrefu kati ya kiungo huyo wa timu ya Taifa ya Rwanda 'Amavubi' na uongozi wa Yanga, hatimaye amerudishwa kundini.

Mchezo wa kwanza wa Niyonzima baada ya mambo kukaa sawa, ulikuwa wa Kombe la Shirikisho (FA) dhidi ya Friends Rangers kwenye uwanja wa Taifa Januari 24 na Yanga kuibuka na ushindi wa magoli 3-0.

Baada ya mchezo huo Niyonzima alirejea rasmi kwenye kikosi cha kwanza cha timu akicheza michezo mitatu mfululizo ya ligi kuu na kutoa mchango mkubwa kwenye michezo hiyo. Nyota huyo aliliambia gazeti hili kwenye mahojiano ya hivi karibuni kuwa amefurahi kwa sasa mambo yamekaa sawa na akili yake imetulia.

"Nina uchu wa kuisadia timu yangu, kwa sasa najiona nina hali mpya ya kufanya vizuri kwenye ligi na hata kwenye mashindano ya kimataifa," alisema Niyonzima.

Alisema kuwa alikuwa akichanganywa na mgogoro kati yake na viongozi wa klabu hiyo, lakini utulivu alionao kwa sasa utamfanya awajibike kwa asilimia zote kwa klabu yake.

"Kikubwa mambo mabaya au niseme kipindi kibaya kimepita, ni wakati wa kuungana kwa ajili ya timu yetu...binafasi naamini tuna nafasi ya kutetea ubingwa wetu, " alisema Niyonzima. KIWANGO Niyonzima ameonyesha bado ana uwezo mkubwa na mchango wa kuisaidia timu yake na hilo alilionyesha kwenye michezo aliyoicheza baada ya kurudi kikosini, ukiwemo mchezo dhidi ya Tanzania Prisons na kumalizika kwa sare ya 2-2.

Pia Niyonzima alichangia upatikanaji wa ushindi wa magoli 4-0 kwenye mchezo wa mwisho wa wa ligi kuu wa Yanga kabla ya kusafiri kwenda Mauritius walipoifunga JKT Ruvu kwa magoli 4-0.

"Tunafanya vizuri nafikiri kutokana na ushirikiano wa wachezaji wote uwanjani, kikubwa nashukuru kocha ameendelea kunipa nafasi kwenye kikosi," anasema Niyonzima.

"Kocha ameniamini na kunirudisha kikosini, hii haimaanishi mimi ni bora zaidi ya wengine hapana, Yanga ina wachezaji wengi wazuri."

AIPOTEZEA SIMBA

"Mimi sioni sababu ya kuihofia Simba, ni timu ya kawaida na tunaweza kuifunga tutakapokutana nayo tena.

" Niyonzima alisema wanachama na mashabiki wa Yanga hawapaswi kuwa na hofu na mchezo huo ujao. Alisema kuwa Simba ni timu kama ilivyo nyingine kwenye ligi na uwezo wa kuifunga wanao.

"Mashabiki wasiwe na hofu na sisi, Yanga ni timu nzuri, Simba ni timu kama ilivyo timu nyingine, hakuna sababu ya kuwa na hofu," anasema Niyonzima akikumbushia mchezo wa mzunguko wa kwanza ambao Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0.

KAMUSOKO, PLUIJM

Kiungo Thaban Kamusoko ambaye aliliziba vyema pengo la Niyonzima wakati walipokuwa kwenye mvutano na uongozi wa klabu yake, aliliambia gazeti hili kuwa, Niyonzima ni mmoja wachezaji bora kwenye ligi.

Kamusoko alisema kuwa Niyonzima ni mchezaji anayenyumbulika na kutoa mchango kwa timu na pia ni msaada kwa wachezaji wengine.

Wakati Kamusoko akisema hivyo, Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm alisema anaamini kwa sasa Niyonzima amejifunza kutokana na makosa na ndiyo maana amerudi kwa kasi kwenye kikosi hicho.

Pluijm alisema kuwa tangu sakata lake lilipomalizika, Niyonzima ameonyesha kujituma kuanzia kwenye mazoezi hadi kwenye mechi.

"Siku zote nasema Yanga ina kundi la wachezaji bora kama Niyonzima ambaye amejifunza mengi kwenye mgogoro wake na klabu," alisema P Picha: T/ Niyonzima picha