Chanjo aliyozindua Rais yajibu makubwa kimataifa, WHO

27Apr 2023
Yasmine Protace
DAR ES SALAAM
Nipashe
Chanjo aliyozindua Rais yajibu makubwa kimataifa, WHO
  • WHO ikimwaga ‘pongezi’ kuu

NADHARIA ya tiba kuhusu chanjo inajulikana na kongwe, ikiwa na nafasi kubwa ya kinga kiafya mtu asiugue. Chanjo kwa jumla, inatajwa kuzuia vifo milioni mbili kila mwaka duniani.

Pale ulipoibuka ugonjwa wa Uviko 19 duniani, nao ukaleta mapya, suala la kinga kupitia chanjo, ikiwa ni zao la watafiti walioumiza vichwa haraka, ukaibua mbinu mpya ya kivita dhidi ya maradhi hayo.

Nchini, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, miezi kadhaa akiwa madarakani mwaka 2021, akishikia vibwebwe baada ya kupatikana misaada ya dawa za chanjo hizo, akaamua kuhamasisha kampeni ya chanjo na uzinduzi wake akaonyesha hadharani, yeye akiwa wa kwanza na watendaji wakuu kiserikali, wakiwamo mawaziri na wakuu wa vyombo va ulinzi na usalama nchini.

Hadi sasa hatua imefika pazuri, kwamba chanjo inapatikana kila mtaa ikiwamo katika zahanati za mitaani binafsi na za serikali, kasi ya Uviko 19 nayo imepungua mno, hata uvaaji barakoa kitaifa unapatikana kwa nadra. Kwa kifupi, kampeni za Rais Dk. Samia kuzindua chanjo imetekelezwa kwa ufanisi na mwitikio ni wa ngazi ya juu.

Tangu kampeni hiyo kuzinduliwa, ripti mbalimbali zakiimataofa zimekuwa zikitokewea kusifu Tanzania kwamba ni kati ya nchi zilizoonyeshja ufanisi mkubwa katika kufanikisha Chanjo ya Uviko 19, barani Afrika salamu zikitumwa hata na Shirika la Afya Duniani (WHO), inayoiwerkia katika. nchi tano bora batrami humo.

Pia, ni siku chache zilizopita, Mwakilishi Mkazi wa WHO nchini, Dk. Boniface Makelemo, ameipongezaa serikali kwa hatua thabiti zinazochukuliwa kupunguza athari za magonjwa yanayozuilika kwa chanjo.

Anasema, WHO na washirika wao wote wa chanjo wanaunga mkono juhudi za serikali na kujitolea rasilimali za watu na fedha, kuinua kiwango cha chanjo kwa watu wote wanaostahili chanjo kwa rika zote.

Kuhusu chanjo ya UVIKO-19, Dk.Makelemo anasema Tanzania imepiga hatua kubwa katika utoaji wa chanjo hiyo,  asilimia 52 ya wananchi wamepata chanjo.

Taarifa ya ofisi ya WHO Tanzania, jijini Dar es Salaam, inasema wakati utoaji wa chanjo dhidi ya UVIKO-19 ukiingia katika hatua ya kuunganishwa na huduma za kawaida, Tanzania imekuwa nchi inayofanya vizuri zaidi kati ya nchi 34 za Afrika zilizokuwa na idadi ya chini ya asilimia 10 ya watu waliolengwa kupata chanjo hiyo hadi Januari 2022.

WHO, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), na Muungano wa Chanjo (Gavi), walizindua Ushirikiano wa Kutoa Chanjo dhidi ya UVIKO-19 (CoVDP) Januari 2022 ili kuwezesha chanjo hiyo kutolewa kwa haraka na kulinda jamii zilizo katika mazingira hatarishi kwa kuchanja watu wake.

Hadi sasa serikiali inaeleza imeweka mikakati ya kuhakikisha huduma za afya hususani za chanjo zinaendelea kuboreshwa, ikiwemo kununua dawa za chanjo unafanyika kwa wakati, ili kuwa na rasilimali za kutosha muda wote na kuongeza majokofu ya kisasa inayoimarisha mnyororo baridi,i kuhakikisha kuwa chanjo zinazotolewa kuwa katika ubora.

Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Tumaini Nagu, katika uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Chanjo Kitaifa yaliyofanyika kwenye uwanja wa Kwaraa mjini Babati, mkoani Manyara, anasema: "Hapa nchini mafanikio ya chanjo ni dhahiri kwa mfano tumefanikiwa kutokomeza ugonjwa wa ndui, magonjwa ya dondakoo, kifaduro, polio na pepopunda.

“Chanjo ni afua (nyenzo) muhimu katika kutokomeza magonjwa na kupunguza vifo hususani vya watoto wa chini ya miaka mitano. Chanjo pia hupunguza gharama kubwa ambazo familia zetu kwa ujumla ingetumia katika kutibu maradhi yatokanayo na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo."

Anafafanua: "Nitoe msisitizo kuwa mtoto yeyote ambaye hajapata kabisa chanjo au hajakamilisha ratiba ya chanjo, ni hatari sana kwa afya yake kwa sababu anaweza kuambukizwa magonjwa na pia ana hatari ya kuwaambukiza wengine sababu hana kinga kamili ya mwili."

"Wiki hii ni mahususi katika kuhimiza familia kuwapeleka watoto wote wanaostahili kupata chanjo katika vituo vinavyotoa huduma za afya vya serikali na binafsi ili wapate chanjo," anafafanua.

Anataja mikakati ya Rais Dk. Samia, ni kuhakikisha huduma za afya hususani za chanjo inaendelea na zinaboreshwa

Kwa upande wake Dokta Nemes Iria ambaye ni Afisa WHO Afya ya Watoto na Chanjo, anatajaManyara ni mkoa ambao ulikuwa nyuma katika utaoaji wa chanjo lakini kwa ushirikiano na serikali ya mkoa wameanza kuzifikia jamii kwa kupeleka wataalamu huku wakiutumia kama mfano katika kupata matokeo chanya

WHO pia imeiorodhesha Tanzania kati ya nchi zilizofanikiwa zaidi Duniani katika utoaji wa chanjo mbalimbali tangu kuanzishwa kwa shirika hilo miaka 75, iliyopita kutokana na mipango thabiti ya serikali nchini.

WHO nchini inasema chanjo nchini  Tanzania imekuwa zaidi kwa  asilimia 2.8, kati ya Januari 2022  na Januari mwaka huu. 

 

Top of Form

Bottom of Form

Top of Form

Bottom of Form