Dk. Sovu anaorodhesha manufaa hayo kwa msemo “safari moja huanzisha nyingine au mkaa bure si sawa na mtembea bure…”
Akaendelea na simulizi namna Aprili mwaka jana Rais alivyorejea na kuzindua filamu hiyo jijini Arusha, shabaha kubwa ni kuitangazia dunia utajiri wa Tanzania.
Hapo Rais Samia akasisitiza kwa kauli: ”Tujitayarishe kupokea wageni kwa kuepusha kutukuwapa usumbufu.”
Kimsingi, ndicho sasa kinashuhudiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi, ambacho sasa kuna mapinduzo ya watalii wageni, takwimu zikiongezeka kila kukicha na asilimia kubwa, ni wanaotoka Marekani, nchi ambayo filamu hiyo ilizinduiliwa, kablaya kuzinduliwa nchini mkoani Arusha.
IDADI YA WATALII
Mhifadhi Daraja la Pili, Hifadhi ya Katavi, Beatrice Msuya, anainisha tamkwimu, watalii wa nje waliotembelea hifadhi hiyo katika kipindi cha miaka mitano, imeongezeka kutoka 266 kwa mwaka 2018/2019 hadi watalii 815 wa sasa.
Kwa mujibu wa mhifadhi hiyo, idadi hiyo 815 ni watalii waliowatembelea kati ya Januari 2023 na sasa, wengi wanatoka Marekani, ambako sinema ya Royal Tour ilizunduliwa.
Pia, Mhifadhi Beatrice anasema, watalii wa ndani katika kipindi cha miaka mitano imeongezeka kutoka 290 mwaka 2018/2019 hadi 2,438 mwaka huu pekee.
YALIYOMO HIFADHINI
Inaelezwa, mtalii anapokea makundi makubwa ya wanyama, wakiwamo viboko, nyati, simba, hata twiga, huku kukipambwa na mandhari tulivu na tambarare yenye nyasi fupi, mabwawa, misitu ya miombo, safu za milima, maziwa na mito inayotiririsha maji.
Ni hifadhi iliyoanzishwa mwaka 1974, ikiwa na ukubwa kilomita za mraba 2,253 na ikaongezwa asilimia 98, mara baada kuunganishwa Pori la Akiba la Rukwa, ikiwa na ukubwa kilomita za mraba 4,471.
Panatajwa kuwa mahali kunakopatikana mti ya mkwaju wenye utamaduni wa kabila Wabende na Wapimbwe, wanaoituimia kwa shughuli za matambiko kwa miaka mingi, ikiaminika inatunza mzimu maarufu kwa jina la Katabi.
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Manendo Peter Maziku, Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Katavi, anasema pana utajiri wa wanyama wengi, mvua za kutosha, mito yenye maji mengi na maziwa mawili; Katavi na Chada inayofikika na kirahisi kwa kutumia usafiri wa barabara, ndege na treni.
Hapo Maziku, anataja hisani na jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza vivutio vya utalii nje ya nchi, kupitia sinema ya Royal Tour, hata imeleta mapinduzi ya wateja wataalii wanaotembelea hifadhi hiyo.
Maziku anasema, wameboresha miundombinu ya hifadhi ikiwamo barabara, eneo la kupumzikia wageni, mabanda ya wageni, pia vyoo kwa wageni.
SIRI YA MAFANIKIO
Mhifadhi Beatrice anataja, pia kuimarishwa doria za ndege na magari hifadhini kumaliza ujangili na uvamizi wa mifugo, huku wakitoa elimu kwa wananchi nje ya hifadhi wanaotumia maji Mto Katuma, kuacha kuyachepushia mashambani mwao.
Lingine anataja ni kuundwa vikundi vya ulinzi shirikishi katika vijiji vinavyozunguka hifadhi, vikishirikiana na askari wa hifadhi.
Vilevile anasema matukuo ya kuvamiwa mifugo, udhibitio wake umeonyesha mafanikio.
Beatrice anadems, Hifadhi Katavi, anataja mikakati yao kukuza utalii, inajumuisha kuitangaza kupitia vyombo vya habari ndani na nje ya nchi, vilevile kwenye maonyesho ya kimataifa.
Anadems, tayari Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Kanda ya Kusini, inayojumuisha hifadhi Katavi, Ruaha na Kitulo, wanashiriki maonyesho hayo kujitangaza.
UJIRANI MWEMA
Mhifadhi Mwandamizi, Francis Kone, anasema Hifadhi ya Katavi, inatoa misaada kwa ajili ya miradi mbalimbali jirani katika miaka mitano iliyopita.
Anadems ni fedha kutoka TANAPA kwa ajili ya kuchimba visima vya maji vijiji vya Sitalike, Igongwe na Matandarari, vyote kila kimoja kikipatiwa Sh. milioni16 (jumla Sh. milioni 48), katika mwaka wa fedha 2017/2018.
Mingine ni jengo la Kituo cha Afya Mwamapuli (Sh. milioni 112), kwa mwaka wa fedha 2018/2019, kisima cha maji kijiji cha Lukima kata ya Majimoto (sh 17.5 milioni), mwaka 2018/2019.
Kuna ujenzi wa vyoo vya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Usevya, sambamba na Sh. milioni 33 za kujenga madarasa; huku ofisi ya walimu Shule ya Msingi Kasegenyama, ina Sh milioni 45 kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
Vilevile, ujenzi wa bweni la wasichana Shule Sekondari Sitalike, uliopokea Sh milioni75 kwa mwaka wa fedha mwaka 2020/2021.
Aidha, anataja hifadhi imeendelea kuhamasisha watu wanaoishi jirani,watembelew hifadhi ili kuwaongezea uelewa wa yaliyomo.
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Sekondari ya Sitalike,wanufaika wa msaada wa hifadhi, Silivester Lameck, anaishukuru TANAPA kupitia Hifadhi ya Taifa Katavi, kwa kuwajengea bweni litawaondolea tatizo la mabinti kutembea umbali mrefu, pia wakiepuka vitendo vya unyanyasaji kijinsia wakiwa shule.
“Tunaishukuru sana TANAPA, wametusaidia sana, kwani bweni hili lina uwezo wa kutumiwa na wasichana 80,” anasema Mwalimu Lameck.
Mmiliki wa Hoteli ya River Side, Juma Kiambile, anasema jitihada za serikali kutangaza vivutio vya utalii, zimesaidia kuongeza utalii wa nje wanaotembelea, Hifadhi ya Katavi, ikilinganishwa na awalihuko nyuma.
Pia, anataja maboresho yaliyowezesha kuwapo barabara ya lami kutoka Mpanda hadi Tabora na Mpanda hadi Mbeya, pia usafiri wa ndege wa uhakika, treni na kufunguliwa na Bandari ya Karema, inayounganisha Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) kumefungua milango ya utalii hifadhini Katavi.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Igongwe, Ephraim Mwambulu, anaishukuru Hifadhi ya Katavi kuanzisha utaratibu wa kufadhili makundi ya wakazi kando ya hifadhi, pia kupatembelea kuona vivutio vyake kila mwaka, ukiwa mpango wa kuboresha uhusiano na jamii.
Anasema amepata fursa hizo kila mara, licha ya akitoka kijiji jirani, lakini anakabaki hifadhini kwa hadhi ya utalii, inamfanya kushuhudia vingi, wakiwamo wanyama wakubwa; simba, chui, tembo na twiga na kuelezwa maisha na tabia zao.
Mfugaji kutoka kitogonji jirani, Kasongwa, anaishukuru Hifadhi ya Katavi kuwapatia elimu ya uhifadhi, hata sasa wanajua umuhimu wa hifadhi kwa nchi, sasa anatoa wito kwa wafugaji wenzake wanaoishi kando na hapo, kuacha kuharibu mazingira.
CHANGAMOTO ZILIZOPO
Hata hivyo, Hifadhi ya Katavi inakabiliwa na matatizo, ikiwamo kukauka mto Katuma wakati wa ukame, unapita ndani ya hifadhi kumwaga maji Ziwa Rukwa, sababu kuu ni wakulima kuchepushia maji mashambani mwao, hali inayowaathiri wanyama.
Mhifadhi Maziku anataja lingine, ni adha ya ujangili wa wanyama, pia kugongwa na magari yanapita katika barabara tatu ndani ya hifadhi, ambazo ni; Sitalike-Kizi, Mpanda-Sitalike-Kibaoni na Majimoto-Inyonga-Sikonge.









