Ulaya yaisaidia Ukraine dola bilioni 5.5

14Mar 2024
Nipashe
Ulaya yaisaidia Ukraine dola bilioni 5.5

MATAIFA wanachama wa Umoja wa Ulaya, yamekubaliana kuipatia Ukraine msaada zaidi wa kijeshi wa dola bilioni 5.5.

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrel.

Ubelgiji ambayo sasa ni mwenyekiti wa umoja huo imesema mabalozi kutoka mataifa hayo 27 wamekubaliana kimsingi juu ya mpango wa kusaidia upelekaji wa silaha nchini Ukraine.

DW imeripoti kuwa, Mchango huo utaingizwa kwenye mfuko unaoratibiwa na Umoja wa Ulaya wa European Peace Facility.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukreine, Dymitro Kuleba ameyaita makubaliano hayo kuwa ya muhimu ya yaliyoafikiwa kwa wakati muafaka.

Uamuzi wa kuongeza ufadhili ulicheleweshwa kwa miezi kadhaa kutokana na mvutano miongoni mwa wanachama juu ya namna utakavyotumika.

Umoja wa Ulaya tayari umetoa yuro bilioni 6.1 kwenye mfuko huo ili kufidia sehemu ya gharama za silaha zilizotumwa na nchi wanachama kwenda Ukraine tangu ilipovamiwa na Urusi.