Kulingana na maelezo ya mwanamke huyo mwenye umri wa miaka (32), mumewe alikuwa akimfanyia kitendo hicho pale anapokuwa amekosea kama adhabu.
Hata hivyo, mpaka kufikia hatua ya Mbwilo kutiwa hatiani na kufungwa, mlalamikaji hakuwahi kufika kortini kutoa ushahidi wake, isipokuwa Mahakama iliamua kuegemea maelezo yake aliyokuwa ameyaandika Polisi.
Hukumu hiyo ilitolewa Machi 6, 2024 na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mufindi, Benedict Nkomola na nakala yake kupatikana Machi 12, ikisema ushahidi uliotolewa umethibitisha mashtaka dhidi ya Mbwilo.
Hakimu amesema katika kesi ya jinai, maelezo ya malalamikaji yanaweza yakatumika kama sehemu ya ushahidi kwa kuwa sheria ya ushahidi inatoa utaratibu wa kushughulika na kesi ambazo mlalamikaji atakuwa hapatikani kutoa ushahidi.