Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro amesema “Awali Jeshi la Polisi lilipokea taarifa za kuibwa kwa mtoto huyo tarehe 06 Februari, 2024 majira ya saa moja usiku kutoka kwa mama wa mtoto huyo aliyefahamika kwa jina la Victoria Charles (34) Mkazi wa Gongo la Mboto, mwizi huyo alijifanya msaidizi wa kazi na baadaye kupata fursa ya kumuiba mtoto huyo”
“Uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi umebaini kuwa mtuhumiwa alimuiba mtoto huyo kwa lengo la kuwaridhisha familia ya wakwe zake baada ya kuwadanganya kuwa alijifungua mtoto tangu mwezi wa Mei, 2023 baada ya kuwa na mahusiano na Kijana wao”
“Mtoto amepatikana akiwa na afya njema na mtuhumiwa atafikisha haraka iwezekanavyo mahakamani ili kujibu tuhuma zinazomkabili, Jeshi la Polisi linatoa wito kwa watu kuwa makini na vijana wa kike wanaojifanya wanatafuta kazi za ndani na baadae kuweza kuwaibia”









