Kundi hilo limeingia jana Februari 24, 2024 ikiwa ni Kazi ya kutangaza Utalii iliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kupitia Filamu ya Tanzania "The Royal Tour".
Imetajwa kuwa watalii hao wametoka katika Nchi za Australia, Austria, Belgium, Canada, China, Ufaransa, Ujerumani, Poland, Urusi na Hispania huku wengine wakitokea Nchi za Switzerland, Uingereza na Marekani wakisafirishwa na Meli iitwayo "Le Bougainville".
Watalii hao wameeleza kufurahishwa na upekee wa historia ya Magofu ya Kale, ustaarabu na utamaduni wa wakazi wanaoishi katika Hifadhi hiyo huku wakipongeza jitihada za dhati za kuboresha miundombinu ya utalii zilizofanywa na Serikali kupitia TAWA Hifadhini humo.
"Imekuwa ni safari nzuri kwetu kwasababu tumepata fursa ya kipekee kujifunza historia ya Nchi hii nzuri ikiwa ni pamoja na kukutana na watu wa tamaduni mbalimbali kuona namna wanavyoimba na kucheza, nimependa sana hakika nimependa" Dominick Alexandre mtalii kutoka Ufaransa
TAWA inaendelea kupokea wageni mbalimbali kutoka Kila Kona ya Dunia kupitia Hifadhi hiyo na Hifadhi nyingine zilizo chini ya usimamizi wake, ambapo katika kipindi cha Mwezi Februari kuanzia tarehe 03 mpaka tarehe 24 Hifadhi ya Urithi wa Dunia ya Magofu ya Kilwa kisiwani na Songo Mnara imepokea Meli za watalii zipatazo sita zikiwa na jumla ya watalii 710 na bado inatarajia kupokea Meli nyingine za watalii ambao watatembelea Hifadhi hiyo.









