Kinana amesema hayo leo wakati wa kongamano la kumpongeza Rais Samia kwa kasi nzuri ya utekelezaji wa ilani ya mwaka 2020/25 iliyofanyika katika uwanja wa CCM mkoa wa Kaskazini Unguja.
Kinana amesema kuna baadhi ya watu wanataka kuvuruga mambo kwa wananchi Rais Samia alipimwa uwezo wake kabla ya kuingia katika nafasi hiyo.
"Huyo anayesema Rais Samia ni wa Katiba sio kweli hao wana ajenda yao tuliupima uzoefu wake bila ya kupewa nafasi na tumeona anaweza na anafanya vizuri," amesema Kinana.










