Kinana ameyasema hayo leo wakati akihutubia katika kongamano la kumpongeza Rais Samia kwa kasi nzuri anayoifanya, lililofanyika Mkoa wa Kaskazini Unguja, akieleza kuwa alipewa nafasi hiyo kwa kuchaguliwa na kwa muongozo wa katiba.
“Tangu Rais achukua uongozi kwenye taifa letu kuna kauli nimekuwa nikiisikia kwamba Rais Samia ni Rais wa katiba, kila chama kinapomchagua mgombea mwenza kinafuata vigezo, hivyo alipimwa na akaonekana kuwa anaweza na anamudu kazi hiyo na anautaratibu mzuri wa kuongoza nchi, anafanya kazi nzuri na tunampongeza,” amesema na kuongeza;
“Wanaosema Rais ni wakatiba hajachaguliwa sio kweli, Rais anapopigiwa kura na makamu wake na yeye ni vivyo hivyo, hivyo Rais Samia alikutana na mchakato wa uchaguzi, wale wanaosema Rais wa katiba msiwasikilize wanaagenda yao,” amesema Kinana.










