Waziri Bashungwa, Kunenge na Dk. Abbas washuhudia Xtra Uni Bash
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Abubakar Kunenge pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Hassan Abbas jana walihudhulia tamasha la Xtra Uni Bash lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa (kulia) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Abubakar Kunenge pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Hassan Abbas wakifuatilia kwa umakini tamasha la Xtra Uni Bash lililoandaliwa na kituo kimoja cha redia na kudhaminiwa na Bia ya Guinness Smooth inayotengenezwa na kampuni ya Bia ya Serengeti pamoja na makampuni mengine. Tamasha hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam jana.